Sunday, May 29, 2022

PEKE YANGU, BALI SI KATI UPWEKE / ALONE, BUT NOT LONELY

 




 


 


PEKE YANGU, BALI SI KATI UPWEKE 

ALONE, BUT NOT LONELY

June 27, 1976 

Pastor Henry F. KULP




 

2 Timoteo 4: 9 – 22 


“Jaribu sana kuja kwangu upesi. Maana Dema aliniacha, akiwa amependa dunia hii ya sasa, na alikwenda hata Tesalonika; Kreske kwa Galatia, Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake ni hapa pamoja nami. Utwae Marko, umlete pamoja nawe; kwa sababu ananifaa kwa utumishi. Lakini Tikiko nilituma Efeso. 

Wakati utakapokuja, ulete joho lile ambalo niliacha kwa Troa kwa Karpo, na vitabu, zaidi vile vya ngozi. 

Alesanduro mfua shaba alinifanyia mabaya mengi: Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. 

Nawe vilevile ujiangalie na huyu, kwa sababu alishindana sana na maneno yetu. 

Katika majibu yangu ya kwanza hakuna mtu aliyesimama pamoja nami, lakini wote waliniacha; lisihesabiwe kwao. 

Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu, ili kwa mimi ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, na Mataifa yote wasikie: nikaokolewa katika kinywa cha simba. 

Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunichunga hata nifike kwa ufalme wake wa mbingu: kwake utukufu uwe kwa milele na milele. Amina. 

Unisalimie Priska na Akila, na watu wa nyumba ya Onesiforo. 

Erasto alikaa kwa Korinto; lakini Trofimo nilimwacha kwa Mileto, mgonjwa. 

Jaribu sana kuja mbele ya wakati wa baridi. Eubulo anakusalimu, na Pude, na Lino, na Klaudia, na ndugu zote pia. 

Bwana Yesu Kristo awe pamoja na roho yako. Neema iwe nanyi.” 

         Mtume Paulo anakuwa sasa mzee, kiisha kuhubiri Habari Njema zaidi ya miaka 30 kufika hadi kiwango cha miaka 35. 

Yeye alifungwa huko Roma katika kifungo nyembamba sana kilichoitwa kifungo cha Mamertimo. 

Kifungo hicho kilikuwa pasipo dirisha iwezayo kumuruhusu kupata hewa  kwa pumzi. 

 Humo ndani, hewa ilikuwa chafu, joto ilizidi mno, hakuwako hata namna ya kutizama mazingira. 

Yote yaliyokuwa mbele ya macho yake ni ukuta na paa ya kifungo hicho kichafu alichokuwa ndani. 


1/ Kwa paa la juu kulikuwa tundu ndogo na ni kwa  hio tundu ndipo walikuwa wakimshushia kila walichokuwa nacho kwa kumpa ale, hata maji ya kunywa yalishushwa kwake kupitia tundu lile ndogo. 

Ilikuwa mahali ya shida na mateso mno. 


2/ Kama vile tutakavyoona, Mtume Paulo aliachwa peke yake, kama vile aya ya 11 hadi 16 inavyosema: Luka peke yake ni hapa pamoja nami.

“Luka peke yake ni hapa pamoja nami. Utwae Marko, umlete pamoja nawe; kwa sababu ananifaa kwa utumishi. Lakini Tikito nilituma Efeso. Wakati unapokuja, ulete joho lile ambalo niliacha kwa Troa kwa Karpo, na vitabu, zaidi vile vya ngozi. Alesanduro mfua shaba alinifanyia mabaya mengi: Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. Nawe vilevile ujiangalie na huyu, kwa sababu alishindana sana na maneno yetu. Katika majibu yangu ya kwanza hakuna mtu aliyesimama pamoja nami, lakini wote waliniacha; lisihesabiwe kwao.” 


3/ Katika hali kama hiyo najuwa kwamba waweza kuwa tayari kuhurumia mtu anayevunjika moyo ama kukosa juhudi. 

Ingeliwezekana kwake kutizama nyuma na kujumulisha kiwango cha miaka yote  aliyotumika ndani ya shida na matatizo  na kuweza kuzania kwamba kazi hiyo haikufurahisha Mwenyezi Mungu, na ni kwa hiyo, yeye anapatikana sasa katika mwisho huu wa matatizo na shida.  


4/ Umbalimbali na hayo, Mtume Paulo hakuwa na mawazo kama yale.

 Kwa kweli yeye aliashwa pekee, lakini hakuwa katika upweke. Hakuna mtu duniani aliyekuwa na furaha kama yeye. 

Bali alitamani sana awe na watu kando yake. 

Aya ya 9, alitamani sana Timoteo aji kwake upesi. Hata vilevile Bwana wetu Yesu Kristo alitamani watu wawe kando yake. 

 Matayo 26: 38 – 40 

“Halafu akawaambia: Roho yangu ina huzuni sana hata kufa; kaeni hapa na kuangalia pamoja nami. 

Akakwenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba akisema: Ee Baba yangu, kama ikiwezekana kikombe hiki kinipitie; lakini si kama ninavyotaka mimi, lakini kama wewe unavyotaka. 

Akakuja kwa wanafunzi wake, akawakuta wakilala, akamwambia Petro: Hamukuweza kuangalia pamoja nami saa moja?”   

 

         Katika shamba la Getsemani, Bwana Yesu alitamani wanafunzi wake wakeshe pamoja naye wakiomba. 

Sisi sote tunatamani watu wawe kando yetu. Jameni niwape aya moja inayochamka mara kwa mara katika mafikili yangu. 


2 Timoteo 4: 17 

“Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu, ili kwa mimi ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, na Mataifa yote wasikie: nikaokolewa katika kinywa cha simba.” 

         Bwana alisimama pamoja nami na akanitia nguvu. 

Yeye alikuwa saa zote daima na uhakika imara kwamba Bwana yu pamoja naye, hakuwa hata siku moja pekee kwa maana Bwana ni pamoja naye. 


5/ Aya ya 4:11 (2 Timoteo 4: 11) 

“Luka peke yake ni pamoja nami. …” 

         Nimekuwa nikijiuliza kwamba eti munakumbuka wakati Luka alijiunga na kundi la Habari Njema? Ilikuwa pale Troa. 

Daktari Luka alikuwa mganga wa kutizama magonjwa kazaa, muniruhusu kutumia mawazo yangu ya kiroho, na ilikuwa siku moja alialikwa ili aende kutunza mugonjwa mmoja, kwa kweli ilikuwa biashara yake kujuwa nyumba kwa nyumba mahali mgonjwa anapoweza patikana, ni hivyo alimpasa kutunza mgonjwa moja aliyetoka kwa muji, akiwa kweli mgonjwa. 

Mtu huyo alikuwa Mtume Paulo. 

Wakati Daktari alipofika kwa makao ya mgonjwa, alimukuta kweli mwenye homa kali, na mgonjwa sana, akigonjwa maleria. 

Jambo ambalo shujaa Mtume Paulo hakuweza kuvumilia, kulazwa kwenye kitatanda.  

 Bali Waroma 8:28, inaambatana sana na tukio hilo.  

“Na tunajua maneno yote yanafanya kazi pamoja kuwapatia mema wale wanaopenda Mungu, kwa wale walioitwa kwa kusudi lake.”

6/ Hali ngumu kwa Mtume Paulo, lakini bahati nzuri kwa Daktari Luka, kwa sababu Mwenyezi Mungu alitumia ugonjwa wa Mtume Paulo kwa kumleta Daktari Luka kwa Bwana Yesu Kristo. 

Mwafahamu neno hili? Mtume Paulo alikuwa na utayari wa kushuhudia yeyote ule aliyekutanana naye.  

Daktari Luka aligeuka kuwa mganga wa kwanza kuwa misionari. 

Alijiunga kwa timu ya kutangaza Habari Njema na Mwenyezi Mungu alimutumia ili Mtume Paulo asonge mbele. 

Yawezekana kwamba kupitia yeye umri wa maisha ya Mtume Paulo uliongezeka.  

Na ni baada ya hapo ndipo aliacha kuwa kandokando ya Mtume Paulo. 


7/ Matendo 16: 10 

“Alipokwisha kuona maono haya, mara moja tulitaka kutoka kwenda Makedonia, kwani tulijua kwa kweli Mungu alituita kuwahubiri Habari Njema.” 

         Angalia sana neno la kuwa na “sisi ama tu”, mwandishi alikuwa kwenye safari akisindikiza mtu mwengine na huyu mtu ni Mtume Paulo. 

 Wakolosayi 4: 14 

“Luka, mganga mpendwa, na Dema wanawasalimu ninyi.” 

         Luka mganga mpendwa. MGANGA MPENDWA. Luka hakuwa tu rafiki wa siku zilizo bora, lakini alibakia akiambatana na Paulo wakati wowote hadi mwisho. 


8/ 2 Timoteo 4: 10 

“Maana Dema aliniacha, akiwa amependa dunia hii ya sasa, na alikwenda hata Tesalonika; Kreske kwa Galatia, Tito amekwenda Dalmatia.” 

         Twapata mtu mwengine anayetajwa hapa, anayekuwa umbalimbali na Daktari Luka. Huyu mtu ni mwenye makosa, ni mtu aliyeachilia huduma. Siyo mtu wa kutumainia. Yeye ni rafiki wa siku zilizo bora tu. 

Alikimbia toka shamba la vita. 


9/ Tuoneshe tabia tatu za mtu huyu: 

9.1 Mwenye kuheshimiwa, hakuna mwenye kuweza kushakia wokovu wake ama kwamba yeye alitumikishwa na Mwenyezi Mungu. 

Filemono aya ya 24, yaonesha wazi:  Alikuwa mutenda kazi pamoja na Mtume Paulo, yeye alikuwa shahidi ya matendo makuu toka kwa Yesu Kristo, yeye alileta mioyo mingi kwa Yesu, hadi hakuna yule aliyeweza kujiuliza kuhusu wokovu wake ama uaminifu wake. 

9.2 Kukimbia huduma 

Kwa sababu gani alimkimbia Mtume Paulo? 

Kwa sababu alipenda dunia hii ya sasa. Mwafahamu? Mapendo ya dunia yalimjaa mno, hadi kumutia kama mgojwa na mapendo yale yalimugeuza kuwa asiye mwaminifu. 

Kupenda dunia ilimuweka mbali na jukumu zake, kwani hakupenda kuvumilia taabu na mateso. 

BALI, WAKATI MTU ANAPOKOMAA KATIKA NEEMA, JUHUDI YAKE YAONGEZEKA, HATA HUJITOA MWENYEWE KWA HUDUMA NA UTAYARI KWA KUTESWA KWA AJILI YA BWANA.

a.   Jaribu kufikiri juu ya vinyume vya hali hii ya kuacha huduma, kwa moyo wa mtume Paulo mwalimu maalum, mchungaji na anaye safari ya kupasha injili. 

Hakuna huzuni kubwa kwa Mtume Paulo sawa kuona mtakatifu wa Mungu, mtu aliye tumikishwa na Mwenyezi Mungu, kurudi nyuma, akitupilia ushujaa wake na kurudi nyuma kwa kufuata dunia. 

Kwa ngambo nyingine ilikuwa kwake jambo la utulivu na furaha kuona Wale watakatifu wanaojitoa roho, nafsi, mwili na akili kutumiki

Bwana, na wanaokomaa katika kiroho na utawa. Jameni, niwaoneshe Maandiko yanayoshuhudia kanuni hiyo 


2 Yoane 4 

“Nilifurahi sana kwa kuona wengine wa watoto wako wanashika njia ya kweli, kama vile tulivyopokea amri kwa Baba.” 

         Mtume Paulo alikuwa akiweka matumaini mengi kwa Dema, lakini sasa yote yalitoweka. 

9.3 Ufunuo gani tunayopata: 

Yafaa tupate mafundisho kwa njia ya uzaifu ya wengine. 

Mtume Paulo hakuwa zaidi ya Bwana wake. 

 

Marko 14: 50 

“Wakamwacha, wakakimbia wote.” 

         Wakati Bwana Yesu alipokamatwa na kupata mapigo akibebwa huku na kule, aliachwa peke yake, wanafunzi wote walimukimbia. 

Naamini kwamba hii ni mapito yenye, kwa nyakati fulani, hukukumba kila mtumishi wa Mungu.

a. Mwenyezi Mungu atuhepushe tusiwe kama huyu Dema. Hakupenda apite kwenye shida na matatizo. Kwa kweli, uaminifu na unyenyekevu kamili una bei gali.

b. Hali mbovu hii haikutukia kwa gafla, bali ilikuwa anguko hatua kwa hatua.

Wakolosayi 4: 14 

“Luka, mganga mpendwa, na Dema wanawasalimu ninyi.” 

         Twaona hapa, yanayoelekea Dema, ni jina lake pekee, yeye si tena mutenda kazi pamoja na Mtume Paulo. 

c. Maana ya kupenda dunia ya sasa ni nini? 

Yaweza kuaambatana na hali ya ukosefu wa azina kwa mtume Paulo. 

Yaweza kumaanisha furaha ya anasa na kujulikana. 

Kutamani kujulikana yaweza kuwa mtego mkubwa sana. 

Kuna awezaye kujizuiza kusema ukweli wake kwa woga ya kupoteza kujulikana. 

d. 1 Wakorinto 4: 18 

“Basi wengine wamejivuna kama kwamba sitakuja kwenu.” 

         Aliinua macho yake na kuangalia dunia ya sasa, akitia mecho juu ya vitu vinavyoonekana pahali pa vile visivyoonekana. 


10/ Yoane Marko ni mufano muzuri kweli: 

Mama yake mzazi alikuwa katika maombi ndani ya nyumba yake ndogo katika usiku ule Mtume Petro alipofunguliwa toka gereza kwa namna ya miujiza.  

 

a. Kwa safari ya injili ya kwanza, yeye alikuwa pamoja na Paulo na Barnaba, lakini, walipofika kwa muji wa Perga huko Panfilia, yeye aliamua kurudi nyumbani kwao Yerusalema, kama vile anavyofanya kila kijana anayebembelezwa na mamaye.   

Yeye alichoka kuendelea kuwa mufuasi wa mtu mwengine. 

Yeye alishindwa na huduma, alikimbia huduma, sawasawa na Dema. 

Baada ya siku chache, kulikuwa safari ingine ya injili na Barnaba alipendelea amuchukue waende pamoja, lakini Mtume Paulo alikataa kabisa. 

Mtume Paulo alifahamu kwamba safari ya injili siyo safari ya kujifurahisha na mazingira. 

Mtume Paulo alikuwa na haja ya mtu mwenye kuwa na utayari wa kuvumilia shida na mateso na magumu ya njia, hapana mtu mwenye ataanza safari na punde kidogo anarudi yake nyumbani, na kwa hiyo alikataa na akasema hapana kwa Barnaba, akimujulisha kwamba Marko hatasafiri pamoja nao. 

Barnaba akiwa ndugu ya Marko, alijaribu kusii Mtume Paulo amupe bahati ya kwenda nao. 

Na hali hii ilisababisha Paulo na Barnaba kutengana, katika hali isiyokuwa ya ushirika. 

Roho zikachafuka sana, Barnaba na Marko wakaelekea Chipra na Mtume Paulo akakwenda pamoja na Sila.   

11/ Watu wengi wanashangaa na kusema: yawezekanaje watu wawili watumishi wa Mungu kubishana hata kufika kiwango cha kutengana. 


Waroma 8: 28 inaambatana kweli na jambo hili. 

Mwenyezi Mungu alitumia utengo huu, sababu Yoane Marko alionesha ya kwamba mahali alipokuwa munyonge na muzaifu, aligeuka kuwa mushindaji na mwenye kutenda yaliyo mema, na hii ni fundisho kwetu tusihesabu watu kuwa hawana faida. 

Yawezekana kwa wakati uliopita hawakufaulu, lakini hii haimaanishi kwamba wao hawataweza chochote kile. 

Mawazo yangu yananikumbusha vile Yona, yeye vilevile kwa mwanzo alishindwa, na alikimbia mbali ya uso wa Mungu. 


12/ Wakati mtu anapokimbia uso wa Mungu, Mwenyezi Mungu anaendelea kumufuata. 

Tazama sasa na furaha gani Mtume Paulo anazungumuza kuhusu Yoana Marko: Utwae Marko, umlete pamoja nawe; kwa sababu ananifaa kwa utumishi. 

 

HATUTAWEZA KAMWE KUJUWA KUSEMA YALE MUNGU ANAYOTARAJIA KUHUSU MTU ALIYEPOTOKA.  

 

Amina. 

 

N°Ref: 06/27/1976 / 299-2 ALONE BUT NOT LONELY / 05/28/2022

No comments:

Post a Comment