Wednesday, September 22, 2021

MKAKATI WA MALAIKA ALIYEANGUKA / THE STRATEGY OF THE MOCK ANGEL


Photo by B Smith from the patio


 

MKAKATI WA MALAIKA ALIYEANGUKA 

THE STRATEGY OF THE MOCK ANGEL 

January 1, 1961

Pastor Henry F. KULP

 

Waefeso 6: 10

“Basi kwa kumaliza, muzidi kuwa hodari katika Bwana, na katika uwezo wake.” Tulikuwa tukizungumuza kuhusu vita kubwa ama mapambano yanayo mkumba mukristo.

Yampasa yeye ndiye awe mwenye kushambulia.

Ni yeye anayepaswa kuongoza na kuleta maelekeo.

Kwa kweli adui wake ni Shetani na mapepo wake wachafu.

Mwenye kustahili kupambana na Shetani katika vita hivi ni mukristo aliye komaa. Hatuwatumi watoto wachanga kwenye vita.

Hatuwatumi vilevile watoto wadogo kwenda kwenye vita, hata mbele ya macho ya Mungu ni hivyo, Mwenyezi Mungu hatarajie watoto wachanga kwenda kupigana vita na shetani, kwa maana, wao hawajuwi ni wapi kuanzia, kwa hiyo yatupasa tukomae kiroho, ili tufike kiwango cha kupambana katika vita na kuwa washindaji.

1/ Shabaa ya Shetani si kwamba tupoteze wokovu wetu.

Shetani anapenda akuibe vifaa vya taji utakayovikwa.

Yeye hafurahie wewe kupata zawabu kulingana na maisha yako ya kikristo.

Maisha ya wakristo wengi yanakuwa na uzembe kuhusu mapambano haya. Kiini yao siyo kujipanga zidi ya kuwa tayari katika mapambano haya.
Wamezarau vita hivi, kwao wamesema wameokolewa na hiyo yatosha kwao, na hii inaonesha lengo ya maisha yao ya kikristo ni ya aina gani.

Wamezarau vita hivi, kwao wamesema wameokolewa na hiyo yatosha kwao, na hii inaonesha lengo ya maisha yao ya kikristo ni ya aina gani.

2/ Tujihazari kufahamu nini iliyo chanzo cha nguvu za watakatifu. Jambo hili ni la maana kweli:
Kwa kuanza mapambano katika vita hivi, yatupasa tuwe wenye nguvu katika Bwana, kuvaa nguvu za Uwezo wake.

Kwa kuanza mapambano katika vita hivi, yatupasa tuwe wenye nguvu katika Bwana, kuvaa nguvu za Uwezo wake.

Neno “kuwa hodari” inamaanisha kuvaa uwezo ama kufanywa kuwa mwenye uwezo. Ni mtu gani anayetuomba tuwe hodari katika Bwana?

Wakati wowote kama unapata mashauri toka mtu fulani, yafaa kweli kujuwa ni nani anayekushauria.

Ni mtu wa aina gani na tabia zake ni gani?

Yeye anaujuzi kweli wa mambo anayokushauria?

Katika ulimwengu huu, ni wengi wanaopenda kupana mashauri hata kwa jambo wasiloelewa vizuri, hawafahamu ni nini wanaosema.

Wanapenda wakushauriye kuhusu namna ya kuongoza jamaa lako, namna gani kulea watoto wako, bima gani kununua kwa niaba ya vifaa vyako, gari gani yafaa kununua, wapi kuishi na mara nyingi wao wenyewe hawakufaulu, sasa wao watakushauri namna gani?

Lakini, tutizame sasa, mtu huyu Mtume Paulo ni nani? Yeye anayetuhimidi tuwe hodari katika Bwana?

Eti yeye alikuwa myonge ama goigoi ama mzaifu? Mimi nina uhakika kama sivyo.

Yeye hakuwa mtu wa hivi hivi.
Paulo alikuwa mtu aliyefahamu maana ya kuwa hodari katika Bwana.
Yeye alikuwa tiyari kwa kupambana vita hivi, na alifahamu kwa uhakika maana ya kuvumilia katika Yesu Kristo.
Yeye alipigwa mawe, alisongwa na maumivu ya vidonda vikali, alifungwa minyororo, alitupwa katika gereza la shimo la chini, lakini alidumu katika mapambano. Wakati alikuwa akihimiza wakristo wawe hodari katika Bwana, yeye mwenyewe alikuwa akipitia katika shida na uchungu mkali.

Paulo alikuwa mtu aliyefahamu maana ya kuwa hodari katika Bwana.

Yeye alikuwa tiyari kwa kupambana vita hivi, na alifahamu kwa uhakika maana ya kuvumilia katika Yesu Kristo.

Yeye alipigwa mawe, alisongwa na maumivu ya vidonda vikali, alifungwa minyororo, alitupwa katika gereza la shimo la chini, lakini alidumu katika mapambano. Wakati alikuwa akihimiza wakristo wawe hodari katika Bwana, yeye mwenyewe alikuwa akipitia katika shida na uchungu mkali.

3/ Wagalatia 6: 17

“Tangu sasa mtu asinisumbushe, kwa maana ninachukua katika mwili wangu

chapa zake Bwana Yesu.” Mtume Paulo asema hivi:

Tangu sasa mtu asinisumbushe.

Hawa watu wa Galatia waliingiliwa na walimu waliowafundisha kwamba mtu yule Paulo si Mtumishi wa Yesu Kristo, yeye siye Mtume, kwa nini kumusikiliza?

Paulo aliwaambia: Munafahamu ya kwamba mimi ninachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu Kristo.

Tufahamu hapa kwamba alitia mkazo akitumia neno “mimi” kwa kujilinganisha na wale walimu wa kiyuda.

Aliwafahamisha ya kwamba, hata kwa wakati anapozungumuza nao yeye anazo chapa za Yesu Kristo katika mwili wake.

Chapa hizo ni gani?

Sababu gani tayari zimewekwa hapa?

Ni vidonda na makovu mabichi, na namna mzuri ya kutafsiri neno “chapa” ni kwa kutumia neno “kovu” na ni hapo tunapopata neno “Unyanyapaa” katika Swahili. Yeye alikuwa kweli na alama maalum.

Kulikuwa makovu na vindonda vya kuumia vya kila nyakati.

Yeye alipigwa mawe, alikuwa na chapa ya vidonda vya kupigwa fimbo, alifungwa minyororo, hayo vidonda, makovu na alama maalum yalionekana wazi mwilini mwake na yalimuhofu sana.

Alama hizo zilikuwa wazi na mbichi mwilini mwake.

Kwa kweli mimi ninaweza kubali mashauri yatokao kwa mtu kama yeye.

Wakati anaponiambia niwe hodari katika Bwana, najuwa kwamba yeye mwenyewe ajuwa maana ya kuwa hodari katika Bwana, pia hufahamu kwamba yawezekana kuwa na hali hiyo ya uhodari.

Yeye ni mtu analiyefaa kupana shauri za namna sawa.

4Mtu aliyetuhimidi tuwe hodari, yeye mwenyewe alikuwa hodari.
Wakati alipokuwa akiandika Maandiko haya, alikuwa akipatikana katika gereza la chimo la chini iliyopatikana kwenye makao ya kifalme.
Bali, huko gerezani, chini ya udongo, yeye alidumu tu akimuhudumia Bwana Yesu Kristo, alikuwa akisonga mbele kwa kupiga vita vema akijitahidi ili apate taji lake. Kuna taji inayoandaliwa kwa yoyote yule atakaye leta nafsi kwa Yesu Kristo.
Yeye alipata taji nyingi wakati bado alipokuwa angali katika gereza ya shimo la chini, yeye alikuwa akishuhudia Yesu Kristo kwa kila mtu aliyekutana naye ndani ya gereza.

Wakati alipokuwa akiandika Maandiko haya, alikuwa akipatikana katika gereza la chimo la chini iliyopatikana kwenye makao ya kifalme.

Bali, huko gerezani, chini ya udongo, yeye alidumu tu akimuhudumia Bwana Yesu Kristo, alikuwa akisonga mbele kwa kupiga vita vema akijitahidi ili apate taji lake. Kuna taji inayoandaliwa kwa yoyote yule atakaye leta nafsi kwa Yesu Kristo.

Yeye alipata taji nyingi wakati bado alipokuwa angali katika gereza ya shimo la chini, yeye alikuwa akishuhudia Yesu Kristo kwa kila mtu aliyekutana naye ndani ya gereza.

Wafilipi 4: 22

“Watakatifu wote wanawasalimu ninyi, zaidi wale walio nyumbani mwa Kaisari”. Mtume Paulo anahakikisha eneo gani? Wale walio nyumbani mwa Kaisari.

Kumbukeni kwamba Mtume Paulo alikuwa katika gereza la chini ya udongo kwa nyumba ya Kaisari, na kweli ni vigumu kukubali kwamba ni katika mahali kama hapo ndipo angaliweza kusubutu kufungua kinywa chake kwa kuzidi tena kushuhudia mbele ya watu wengine wa nyumba ya Kaisari, lakini kwa kweli yeye alifanya hivyo.

Kwa kweli Neno aliloshuhudia liligusa na kukomboa nafsi za wafanyakazi wa ndani ya nyumba, waaskari, na hata vilevile wamoja wa Wakubwa wa waaskari, na yawezakana, humo ndani waliunda hata kanisa ndogo, ama muungano wa waamini waliokuwa nyumbani mwa Kaisari.

Yeye alipambana vitani hadi mwisho.

Kweli ni wajibu wangu kumusikiliza mtu kama huyo.

NINAWEZA KUKOKOTA KITI CHANGU NA KUKARIBISHA SIKIO LANGU ILI NISIKILIZE SIRI YA HIYO NGUVU.

5Kwa kweli, ombi la kutuhimiza tuwe hodari katika Bwana lafwatana na lingine linalotuomba kwamba:
Tuvae silaha zote za Mungu, tupate kuweza kupinga hila zote za Shetani. 

Tuvae silaha zote za Mungu, tupate kuweza kupinga hila zote za Shetani. Waefeso 6: 11

“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kupinga hila zote za Shetani.” Fahameni kwamba hapa kuna mupinganizi.

Mupinganizi wetu ametajwa, yeye ni Shetani na silaha zake zinajulikana kwamba ni hila.

Tujifunze kwa makini mpinganizi wetu, ili tufahamu namna gani tupasalo kupambana vitani humo.

Mara nyingi tunayo mawazo ya kuzania kwamba vita tunavyo ni vya mwili na damu, dada zetu na kaka zetu katika nyumba, rafiki katika jamii, majirani katika mtaa mpana, washirika wetu katika biashara, huyo mtu anayetuletea migorogoro na shida nyingi katika nyumba.

Tufahamu sana kwamba vita vyetu si vya damu na mwili.

Kweli mwili na damu yaweza kutupitisha kwenye majaribu makali sana, wajirani vilevile wanaweza kuchekelea hali yetu.

Hata mara nyingine wapendwa wetu katika jamaa, waweza kuwa na mume ama muke anayechukia upendo wako kwa Bwana Yesu Kristo na namna unavyomuzingatia. Waweza kuwa na watoto wenye hawaheshimu lile unalowaamuru watende, na vivi hivi. Bali mapambano tunayo maishani mwetu, si hiyo. Kwa kweli.

6Tufahamu kwa makini kabisa kwamba hatushindani na damu na mwili, ila tunashindana na Shetani na majeshi ya wafuasi wake mapepo wabaya.
Taswira na wazo tunayo hapa ni magonvi ya kupambana mwili kwa mwili, tukiwa mikono mitupu.

Taswira na wazo tunayo hapa ni magonvi ya kupambana mwili kwa mwili, tukiwa mikono mitupu.

Wagriki walifahamu kabisa kabisa wakati Mtume Paulo alipotumia neno kushindana. Ilikuwa vita na ugonvi mwili kwa mwili, kila mmoja akitumia nguvu zake zote ili amugandamize mwenzewe na kumutupa chini.

Katika mashindano haya, mshindi anagandamiza mwenzake akimufinyanga kwa udongo na, katika aina ya ugonvi huu wa kigriki, mecho ya yule aliyeshindwa yaweza kutobolewa na kuwa na bahati mbaya ya kubaki kipofu kwa maisha yake yote, naamini kwamba kwa mwangaza wa picha hii munafahamu namna gani wakristo wa Efeso walitambuwa vita gani Mtume Paulo alionesha wakati aliandika neno kushindana.

Siyo jambo la mizaa, siyo mambo ya hivihivi, lakini ni vita ya hofu kubwa.

7Tukifahamu jambo hili vichwani mwetu, tusome sasa aya ya kumi na moja (11): Ya tuambia kwamba tuvae silaha zote za Mungu, ili tupate kuweza kusimama juu imara, hapana kutupwa chini na kuanguka, tusigandamizwe chini kwa udongo, lakini tuweze kusimama imara tukishindana na nguvu za hila za Shetani.

Neno hila, inamaanisha namna ya kutenda ya uerevu na ujuzi maalum, ama waweza kutumia neno Mkakati.

Shetani atumia mkakati ya ujuzi maalum kwa kushindana nasi.

Ingekuwa raisi sana, sawa michezo ya kitoto, kama Shetani angaliweza kujitokeza mbele yetu na kusema: Amjambo, mimi ni Shetani na vivi hivi.

Mimi ni mjumbe wa kazi za giza toka kwa bwana wangu Diabolo, na mimi nitahitaji wewe ukubali kuingia katika jambo hili lenye litakuletea mateso, hofu na shida

kubwa, umasikini na kumukana Mwokozi wako, na kuharibu hata ushuhuda wako, ni wajibu wako kunisikiliza tu ili mambo haya yote yatimie.

Kwa upesi sana tungejibu: Uwe mbali sana nami ewe Shetani, sitaki hata jambo moja toka kwako, na sina uhusiano nawe, ondoka.

Bali, shetani hatumike namna sawa.

Majeshi wake pepo wabaya hawatumie uendeshaji wa namna sawa.

Tunapata mfano muzuri katika Kitabu cha Yosua sawa sawa na namna nilihitaji tufahamu.

Kumbukeni namna tulivyowaambia kwamba Kitabu ya Yosua katika Agano la Kale inalinganishwa na Kitabu ya Waefeso katika Agano Jipya.

8Mwenyezi Mungu alimuhimidi Yosua atambuke mto Yordani, na kwamba ni kwa pwani la ngambo ndipo atakapokuta Inchi yenye Mungu alimupa, mahali kunako Taifa saba ya wa Kanana.
Ilikuwa mataifa yenye kujaa ukorofi, uchafu wote, yenye laana na kuabudu miungu, na Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba wasiwe na uhusiliano wowote na taifa zile, wasioane nao, bali wawaangamize, wawaangamize wote bila kubaki hata mmoja wao. Maagizo yalikuwa waziwazi na Yosua na Taifa nzima walikuwa wakiyaheshimu sawa sawa na namna Mwenyezi Mungu alivyowaahidi, hadi hapo.

Ilikuwa mataifa yenye kujaa ukorofi, uchafu wote, yenye laana na kuabudu miungu, na Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba wasiwe na uhusiliano wowote na taifa zile, wasioane nao, bali wawaangamize, wawaangamize wote bila kubaki hata mmoja wao. Maagizo yalikuwa waziwazi na Yosua na Taifa nzima walikuwa wakiyaheshimu sawa sawa na namna Mwenyezi Mungu alivyowaahidi, hadi hapo.

Siku moja kulikuwa umati wa wageni wamoja waliokuwa wakivikwa nguo za kuchakaachakaa na zenyi tayari zimekwisha pasukapasuka, watu hawa walikuwa wakitembea polepole kwa barabara kubwa.

Walikuwa wakivaa viatu vya kambakamba kwenye miguu yao na mikononi mwao walikuwa na ndaa ndogo zikiwemo mikati yenye imekwisha kuozana walikuwa pia na vibuyu vya maji vilivyojengwa na ngozi ya mbuzi vyenye tayari vimekwisha pia kuchakaa na kutobokatoboka, na vikavu.

Kiisha wapelelezi wa Yosua wakakwenda kukutana nao na kuwauliza: wao ni wanani na wanahitaji nini?

Waliwajibu ya kwamba wanahitaji kumwona Akida mkuu wao.

Na wakati walipopelekwa mbele ya uso wa Yosua, Yosua akawauliza: Munataka tuwafanyie nini pia munatoka wapi?

Walijibu kwamba:

Kama vile hali ya mavazi yetu yaonesha, sisi tunatoka kwa muji wa mbali sana, vazi zetu zilikuwa mpya kweli siku tuliacha nyumba zetu na kuanza safari, mwaweza kutambuwa kwamba tulifanya safari ndefu.

Viato tunavyo kwa miguu yetu, tuliviuza toka muuzaji mmoja siku tuliyoondoka na kuanza safari yetu, mwaona sasa katika hali gani vinakuwa leo, vikichakaa na kupasukapasuka.

Na mikate haya yalikuwa yakitoka kwa tanuri, lakini sasa yameoza.

Sisi tunatoka safari ya mbali sana tukitembea, sababu tulisikia habari yenu toka mbali, namna gani huyo Mungu yuko pamoja nanyi, kwa hiyo tulitamani tufanya ushirikiano pamoja nanyi.

Eti, mwakubali tuwe marafiki?

Ni jambo la heshima kwetu kuungana pamoja nanyi, kwa hiyo twawaomba tafazali, tufanye patano la ushirikiano pamoja nanyi.

Yosua akasema, kweli hii ni jambo la kushangaza.

Yawezekana je, kufwatana na eneo kubwa hili la jangwa linalotutenga, nyinyi musikie habari zetu namna gani?

Wakajibu: Oh habari zenu zilitambaa na kuenea dunia nzima.

Tulisikia namna gani muliingia na ushindi wakati mulipofika katika mahali hii, namna gani Jeriko na Ayi zilianguka mikononi mwenu, bali kwa sasa tafazali tuungane na tufanye patano la ushirikiano.

Ni namna hiyo ndiyo twasoma kwamba watu wale walifanya mapatano nao, na bila kumuuliza Mwenyezi Mungu mashauri.

Yosua 9: 14 - 16

“Watu wakachukua chakula chao na hawakuuliza shauri kwa kinywa cha BWANA. Yosua akafanya salama nao, akafanya mapatano nao ili kuwaacha hai, wakubwa wa makutano wakawaapia.

Ilikuwa kwa mwisho wa siku tatu nyuma ya kufanya mapatano nao, wakasikia ya kama walikuwa jirani za karibu nao, wakakaa katikati yao.”

Kwa hiyo walidanganywa na hila za mkakati za wa Gabaoni, baada ya kufanya mapatano nao kiisha siku moja ama miwili, wakati haikuwa tena raisi kuyavunja ni hapo sasa ndipo walitambua kwamba watu wale walikuja toka mungini iliyo jirani na kwahiyo walipenda kwa shali ama kwa mema waungane na kufanya salama nao ili waponeshe nafsi zao na kubaki hai.

Hiyo ndiyo picha ya matumikio ya Shetani na malaika wake pepo wabaya wanapojiingiza katikati ya wana wa Mungu.

Wanatumia mbino za wajuzi, hawajitokeze namna wengi wanavyozania.

9/ Watu wanaweza sema kwamba mtu fulani iko anakwenda kuona mashetani. Wao hawatambui kwamba shetani hana lakufanya na maneno ya namna sawa. Siyo kosa lake.
Sasa Shetani anakuja namna gani?

Sasa Shetani anakuja namna gani?

Tunayo zoezi ya kutumia Maandiko Matakatifu bali, mpaka hapo, watu hawana ufahamu.

2 Wakorinto 11: 3

“Lakini ninaogopa, ya kwamba sawasawa nyoka alivyodanganya Hawa kwa hila yake, mawazo yenu yataharibiwa, na mutaacha weupe wa moyo na usafi katika Kristo.” Hapa Mtume Paulo anasema ya kwamba:

Sawasawa namna mawazo yenu yanaharibiwa na munaacha weupe wa moyo na usafi katika Kristo, na kwa kweli anayefanya hivi ni Shetani, Diabulo.

Weupe wa moyo na usafi katika Kristo.

Ni waamini wengi wasioshikamana na weupe wa moyo na usafi katika Kristo. Wanapenda kuonesha kwamba ni vigumu sana kuishi katika hali hiyo.

Kwa kweli ingekuwa faida, kwa musaada wa Roho Mtakatifu kufikia kutimiza lengo la kuishi ndani ya hali hiyo.

Kwa kweli ingelikuwa heri kuipambanisha na mambo mbalimbali ya maisha ya kila siku. Ingelikuwa heri kuwa na hamu ya hali hiyo.

Ingelikuwa heri kuwa na tabia ya maisha mazuri, pahali pa kusadiki Yesu Kristo kwa Imani tu, ila kujitahidi siku kwa siku kumtazamia tu Bwana Yesu Kristo, roho ikijaa na Neno la Mungu.

Siyo mshangazo kuona Shetani akiwashinda wakristo wa desturi akiwaangusha na mbino za hila zake.

Anafanya hivyo kwa njia gani?

Shika jambo hili kwa makini sana: Kwa njia ya nia ya mawazo, Shetani hutumia njia hii ya mawazo, ni lazima na muhimu kufahamu jambo hili.

Shetani anatumikisha mafikili, ama mawazo ya mwamini, mapambano haya ya ugonvi wa mwili kwa mwili ufanyika katika nia ama mafikili.

10/ Tuchunguze sasa namna Shetani anavyotumika:

2 Wakorinto 11: 13 – 14

“Maana hawa ni mitume ya uwongo, wenye kutenda kazi kwa hila, wakijigeuza wenyewe kuwa kama mitume ya Kristo.

Wala si ajabu; kwa sababu Shetani mwenyewe anajigeuza awe malaika ya nuru.” Anajigeuza mwenyewe awe malaika ya nuru. Yeye haje kwa njia ya ukali. Anajileta kwa wema wa kibinadamu, kama malaika wa nuru katika nia na mawazo yako.

11/ Tuchunguze Maandiko mengine yanayotupatia taswira ya mapambano na vita yetu:

2 Wakorinto 10: 3, 4

“Kwa maana hata tunatembea katika mwili, hatufanyi vita kwa namna ya mwili; (Maana silaha za vita yetu si za mwili, lakini zina uwezo katika Mungu kuangusha maboma ya vita);”

Tunaambiwa mara tena ya kwamba sisi tunatembea katika mwili, bali vita vyetu si vya mwili hata kidogo.

Kwa sababu silaha za vita vyetu si vya mwili, lakini vina uwezo katika Mungu kuangusha maboma ya vita, inamaanisha kwamba vitani mwetu twapashwa kugandamiza adui, twapashwa kumuangushia silaha zetu nzito Sawa sawa na namna adui alivyofanya hapo kale.

Wakati walipopenda kuzingira mahali kwa kuishika, waliizunguuka pande zote, wakishika na kufunika milango yote na ni hapa sasa walipashwa kuangusha maboma. Je ni maboma gani?

Ni maboma gani yanayopashwa kuzingira?

Ni mawazo, mafikiri, na kuweka kila nia na mawazo kwa utumwa chini ya

kutii Kristo.

Kiisha kuyashinda na kuvunja mawazo na mafikiri, ni nini inayotegwa nyara na kushikwa?

Yanayoshikwa ni mawazo.

Tunapigwa vita na Shetani katika nia na mawazo yetu na mapambano hayo ni ya ana kwa ana.

12/ Wakolosai 3: 2

“Tieni mafikiri yenu juu ya maneno ya juu, wala si juu ya maneno yaliyo duniani.” Tumeambiwa hapa kwamba tuweke mafikiri yetu juu ya maneno yaliyo juu. Hatupashwi tu kutarajia kwenda mbinguni na kutafuta mbingu, bali mafikiri yetu yapashwa kuelekea mbingu.

Nikusema kwamba neno “kutamani” yamaanisha mafikiri ama mawazo Tunapashwa kuwa na mawazo yenye saa zote yafikiri tu mambo ya mbinguni siyo mambo ya duniani.

Twapashwa kufikiri Kristo, hii ndiyo vita vyetu.

Wakati tunafikiri Kristo, Shetani na majeshi zake mapepo wachafu wanahitaji tufikiri maneno mengine pahali pa kufikiri Kristo.

Maneno yale na vifaa vile kweli vyatufaa maishani mwetu, bali vifaa vile na maneno yale siyo ya Kristo, na ni hiyo vita tunavyo.

13/ Wafilipi 4: 8

“Kwa kumaliza, ndugu zangu, maneno yo yote yaliyo ya kweli, maneno yo yote yaliyo ya heshima, maneno yo yote yaliyo haki, maneno yoyote yaliyo safi, maneno yo yote yenye kupendeza, maneno yo yote yenye sifa njema; ukiwa wema wo wote na ikiwa sifa yo yote fikirieni maneno haya.”

Ningetamani muweke mukazo kwa maneno mawili hapa:

Katika aya ya nane tunaambiwa kuwaza haki sambamba yenye haki.

Na katika aya ya kenda twaambiwa kutenda haki.

Ni kusema kwamba ukiwa na mawazo sambamba yenye haki, kwa urahisi wote utatenda haki.

Hii ndiyo jambo la musingi, utaratibu wa kinidhamu katika mafikiri yetu. Kweli tutaambatana na kufanana na yale tunayofikiri.

14/ Waroma 12: 1 – 3

“Kwa sababu hii, ndugu, ninawasihi ninyi, kwa rehema za Mungu, mutoe miili yenu iwe zabihu iliyo hai, takatifu, ya kupendeza Mungu, ndio utumishi wenu ulio na maana. Na musifananishwa kwa namna ya dunia hii; lakini mugeuzwe kwa kufanya upya nia zenu, mupate kujua sana mapenzi ya Mungu, yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

Kwa sababu kwa neema niliyopewa, ninamwambia kila mtu wa kwenu, asiwaze kujisifu kupita ilivyompasa kuwaza, lakini awaze kwa akili, kama Mungu alivyogawia kila mtu kadiri ya imani.”

Tambueni kwamba ni haya Shetani hatamani nyinyi kufanya.

Kumtia Mwenyezi Mungu mbele ya maneno yote, kujitowa wewe mwenyewe kwa Mungu kama sadaka iliyo hai.

Shetani hapendi jambo hili, kwa hiyo anahitaji nini?

Anahitaji kupotosha mafikiri yako isifikiri namna sawa, ndiyo maana Mwenyezi Mungu anatuomba tugeuzwe kwa kufanya upya nia zetu, na wakati nia yako inafanywa upya, wewe utakuwa na akili na utajiwaza na kujiona sawasawa na ginsi inavyokupasa kuona utu wako, hauta kuwa mwenye kiburi na kujisifu.

Wewe hautajiona kuwa juu ya wengine na kuwa mwenye nguvu na uwezo wote kupita wengine.

AMINA

N°Ref: 01/01/1961 / 28 - THE STRATEGY OF THE MOCK ANGEL / 09/22/2021

Monday, September 6, 2021

ETI NI WATU WOTE WATAKAO OKOLEWA? / WILL ALL MEN BE SAVED?

Photo by B Smith from the patio


 


ETI NI WATU WOTE WATAKAO OKOLEWA? 

WILL ALL MEN BE SAVED?

November 11, 1962

Pastor Henry F. Kulp 


 

1 Timoteo 2: 1 – 4 


“Basi ninaonya mbele ya maneno yote, kuomba, na kusihi, na kuombea, na kushukuru kufanyike kwa ajili ya watu wote; kwa wafalme na kwa wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya kimya na salama, katika utawa wote na upole.

Kwa sababu hii ni nzuri na la kukubaliwa mbele ya Mungu Mwokozi wetu; anayetaka watu wote waokolewe na kupata kujua sana yaliyo kweli.” 

Kuna mafundisho yanayovuma katika ulimwengu kwa siku za leo,na ni udanganyifu ya kuhamakia ili kuhepuka kutupwa  kwenye shimu la jehenamu. 

Ninahuzunishwa sana na kushangaa namna gani watu wanavyoweza kusadiki mafundisho yale, sababu hakuna hata aya moja ya Maandiko Matakatifu ya Biblia inayo tetea mafundisho ya namna ile. 


1/ Ni mafundisho gani yanayosambazwa ulimwenguni kwa siku za leo? 

Ni upatanisho kwa watu wote, inayotambulikana kwa jina la 

Kilimwengu ama ulimwengu wote. 

Zehebu hilo linaitwa Kilimwengu ama ulimwengu wote na mwenye kushiriki zehebu hiyo anaitwa wakilimwengu ama waulimwenguni wote. 

Bali zehebu hiyo inajulikana kwa jina la Upatanisho wa ulimwengu wote.

 2/ 2 Wakorinto 11: 14 

“Wala si ajabu; kwa sababu Shetani mwenyewe anajigeuza awe malaika ya nuru” 

Shetani anatajwa hapa, kama mwenye kuchochea wakristo wazembe akiwaonyesha matarajio yasiyo ya kweli ili awagandamize na kuwatenga wasisikie na kufuata ukweli ulio ndani ya Kristo Yesu, kwa hiyo, kujigeuza kwake kama malaika wa nuru kwa siku za leo na katika siku zilizo pita, ni katika mafundisho hayo ya upatanisho ya ulimwenguni mwote, sababu mafundisho yale yanakuwa sawa yaliyo mazuri kwa kusikia na yenye kubembeleza hadi wengi wanayakumbatia na kuanguka ndani.  

Ila, yote ni udanganyifu mtupu wa shetani toka mwanzo hadi mwisho. 

3/ Watu wale wanatumia Maandiko kama: 

1 Timoteo 2: 4  

“anayetaka watu wote waokolewe na kupata kujua sana yaliyo kweli.” 


2 Petro 3: 9 

“Bwana hakawii kutimiza ahadi yake, kama wengine wanavyozania kukawia; lakini ni vu 


1 Yoane 2: 2 

“naye ni kipatanisho kwa zambi zetu; wala si kwa zambi zetu tu, lakini kwa zambi za ulimwengu wote.” 

Wakitumia Maandiko yale ile wafundishe kwamba kwa mwisho watu wote wataokolewa, na Kristo ni wa watu wote.  


Tutambuwe kwamba 1 Yoane 2: 2 inasema kwamba:

Yeye ni kipatanisho kwa zambi zetu; wala si kwa zambi zetu tu, lakini kwa zambi za ulimwengu wote.” 

Mwenyezi Mungu hapendi hata mtu mmoja kupotea na watu wale wanatumia kwa ujanja aya moja kwa moja. 


4/ Mwenyezi Mungu haja ahidia bado kwamba watu wote wataokolewa. 

  Muniruhusu niwafahamishe kanuni moja inayopatikana mahali mbalimbali katika Biblia:  


Matayo 7: 13, 14 

“Ingieni kwa mlango ulio mwembamba; kwani mlango ni mpana na njia ni pana inayokwenda hata upotevu, nao ni wengi wanaoingia kwa mlango huu. 

Lakini mlango ni mwembamba, na njia imesonga inayokwenda hata uzima, nao ni wachache ambao wanaiona.” 

Hapa, katika mahubiri juu ya mlima Bwana Yesu Kristo anasema: 

 Ingieni kwa mlango ulio mwembamba; kwani, mlango ni mpana na njia, fwateni vizuri hapa, ni pana inayokwenda hata upotevu, hapana hata wokovu. 

Kiisha anatumia neno: nao ni wengi wanaoingia kwa mlango huu. 

Tuchunguze sana neno: Wengi na Upotevu.  

Kiisha kwa aya ya 14 anasema: 

Lakini mlango ni mwembamba, na njia imesonga inayokwenda hata uzima, nao ni wachache ambao wanaiona.” 

  Namna gani twaweza kuzania jambo la upatanisho wa kiulimwengu katika aya hizi tunazo zisoma? 


5/ Naamini kwamba munajiuliza ni kitu gani kinachotuma mafundisho yao yawe mabaya sana na yenye laana? 

Ni kwa sababu yanamutwiga Mungu china ya zambi. 

Na ni hiyo msingi wa mafundisho yao. 

Katika mafikara yao wanaweka china la zambi ndani ya roho na mawazo ya Mwenyezi Mungu. 

Wanasema ya kwamba ni Mungu mwenyewe aliyoyaunda na kuyaleta kwa faida ya mtu na kwa sifa yake Mungu mwenyewe. 

 Wanasema kwamba zambi iliingia duniani kwa njia ya Mungu. 

Na Yeye aliileta kwa kusudi la kuboresha miradi yake ya neema, ili apate kuokowa watu wote. 

Bali, Mwenyezi Mungu Yeye mwenyewe husema nini kwa ajili ya mambo haya? 

Eti ni yeye aliyeleta zambi katika dunia? 

Eti ni yeye aliyeunda zambi katika mawazo yake, ili baadaye nyinyi muokolewe kwa njia ya neema yake? 


6/ Kuna Andiko moja ya Biblia inayoleta uvuguvugu kwa hawa watu wa Kilimwengu. 


Mwanzo 6: 5, 6   

“Bwana akaona ya kama uovu wa watu ulikuwa mkubwa duniani, na ya kama mawazo yote ya mafikiri ya mioyo yao yalikuwa mabaya tu siku zote.  

Fanya sasa angalisho hapa:

Na Bwana alijuta ya kwamba amefanya watu duniani, ikamhuzunisha moyoni mwake.” 

Eti neno hili yaambatana na mafikiri ya kusema ya kwamba ni Mwenyezi Mungu aliyeunda zambi, na kuiingiza duniani kwa niaba ya Neema yake? 

Ni nini hawa watu wa kilimwengu waweza kufanya na Andiko kama hili? 


7/  bKuna vile vile Andiko lingine la Biblia lenye kukoroga hawa watu wa Kilimwengu. 


Yeremia 32: 35 

“Tena walijenga pahali pa juu kwa Bali, palipo katika bonde la mwana wa Hinomu, ili kupitisha wana wao na binti zao katika moto kwa ajili ya Moleki, nisivyowaamuru, wala halikuingia katika moyo wangu kwamba watende chukizo hili; wapate kukosesha Yuda.” 

Anasema ya kwamba, pale Tafa, wao walijenga pahali pa juu, ili kupitisha wana wao na binti zao katika moto, jambo lenyi sikuwaamuru, wala halikuingia katika moyo wangu. 

Mwenyezi Mungu hakufurahia zambi kufika katika ulimwengu, Yeye hakuunda zambi katika mafikiri yake kwa niaba ya neema. 

8/ Watu wa Kilimwengu wanafundisha ya kwamba hukumu ya zambi haiko juu ya mtu na wanatia mzigo wote wa zambi kwa Mwenyezi Mungu.  

Wanafundisha kwamba Mwenyezi Mungu aliweka  kati bustani, mti wa kujua mema na mabaya kwa kusudi la kumjaribia mwanadamu kwa kumusukuma kwa kutenda zambi, ili baadaye,  Mungu aje na Neema yake kwa kuokoa mwanadamu.  


Lakini wao wanasahau Maandiko katika Biblia iliyo wazi kweli na inayosema:  


Yakobo 1: 13 

“Mtu akijaribiwa, asiseme: Ninajaribiwa na MUNGU: maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hajaribu mtu.” 

Mwenyezi Mungu anasema hapa kwamba: 

Mtu yeyote akijaribiwa, asiseme: Mimi ninajaribiwa na Mungu, maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala Yeye mwenyewe hajaribu mtu. 

Ni kweli kwamba ni Mwenyezi Mungu ndiye aliyetia mti wa kujua mema na mabaya katika bustani, na haikuwa kwa ajili ya kujaribu ili mtu ale tunda la mti huo, lakini ilikuwa kwa kuhimarisha uhusiliano kati ya Mungu na mtu, sawa na kiumbe na Muumba wake, ili mwanadamu atende tu yale Mungu anayomuomba kutenda. 


9/ Kama ingelikuwa kwamba ni Mwenyezi Mungu aliyesukuma mwanadamu kutenda zambi, basi Adamu angelikuwa na singizio kamilifu wakati alipohukumu muke wake na kusema kwamba ni yeye aliye chanjo na wajibu wa zambi Adamu alilofanya, akisema: “Mwanamuke ambaye ulinipa awe pamoja name.”  

Eti Mungu hakuwa na haki ya kumuhukumu? 

Hapana kweli, mwanadamu alikuwa na uhuru wa kuchagua. 

Na Mungu hakumtuma mtu kuchagua zambi. 


Mwanzo 3: 12 

“Mwanamume akasema: Mwanamuke ambaye ulinipa awe pamoja nami, yeye alinipa ya mti, na nilikula.” 

10/ Wakati unaposoma kawaida ya mafundisho yale, ama mtu yeyote kukuzungumuzia juu yake, pale pale kuna Maandiko ninayo kumbuka katika mafikiri yangu: 

Yobu 1: 22 

“Katika maneno haya yote Yobu hakukosa wala kushitaki Mungu kwa upumbafu.” 

Ndugu zangu, kumutwiga Mungu wajibu wa zambi iliyo ilimwenguni ni neno la upumbafu na lenye laana. 

Yobu hakufanya zambi wala kusingizia yeyote kwa upumbafu. 

Ni kwa upumbafu ndiyo mafundisho yale yanamuhukumu Mungu. 

Mwenyezi Mungu hana wajibu wowote juu ya zambi zetu. 

Mungu hajaribu wanadamu ili watende zambi. 

11/ Acheni tuwaoneshe Maandiko mbali mbali yenye watu wa kiulimwengu wanatumia ili wahakikishe kwamba siku moja watu wote wataokolewa, wakishuhudia kwamba Neno la Mwenyezi Mungu inatangaza uhusiano wa ulimwengu wote. 

Yoane 12: 32  

“Nami kama nikinyanyuliwa juu ya dunia, nitakokota watu wote kwangu.” 

Ya kwaza ni kwamba Maandiko haya hayasemi ya kwamba Bwana Yesu atakokota watu wote kwake kwa niaba ya wokovu. 

Watu hao wanamemba wanaotangaza habari za uhusiano wa kiulimwengu, wao hawaamini kwamba Yesu Kristo ni Mungu. 

Wanakanusha Umungu wa Yesu Kristo na ni jambo hili inayotia mafundisho yao yawe ya laana na lenyi kukufuru. 

Kama ungelikuwa na bahati mbaya ya kuwasikiliza utatambuwa kwamba wao wanasema kwamba katika Maandiko haya, Bwana Yesu ni mwenye  kujionyesha na hali  tukufu ya juu sana. 

Na kwamba kilichomukosa ni kusema ukweli. 

Wakati aliposema: Mimi ni Kweli. 

Akisema: Nami wakati nitanyanyuliwa juu ya dunia, nitakokota watu wote kwangu. 


12/ Tuchunguze kwanza sehemu hii: Nami kama nikinyanyuliwa.  

Ni nini anayozungumuzia hapa? 

Bwana Yesu anazungumuza kuhusu Kufa kwake kwa Musalaba wa Kalvari.  

Mutatambua kwamba haihusu huduma aliyohudumia watu, ama siyo mafundisho yake iliyokuwa na uwezo wa kuwavuta watu kama asmako, lakini ni Kufa kwake kunaokuwa na uwezo wa kuvuta watu kwake kama asmako. 


13/ Tuzungumuzie sasa neno: Kukokota.  

 Neno hili linatumiwa mara tano katika Kitabu cha Yoane, na mara moja katika kitabu cha Matendo ya Mitume. 

Na wakati wowote neno kukokota inatumikishwa, inamaanisha kukukota kwa kutumia nguvu, ni kusema uwezo unao gandamiza, neno hilo limetumikishwa katika Yoane 21: 11 

“Basi Simoni Petro akaingia chombo, akakokota wavu hata pwani, umejaa samaki wakubwa mia moja makumi tano na watatu; na hata walikuwa wengi hivi, wavu haukupasuka.” 

Hapa ni kwamba ndani ya wavu munaonekana samaki wakubwa mia moja makumi tano na watatu, na samaki hizi zapatikana ndani ya wavu wakati wavu inakokotwa pwani. 

Samaki walikuwa ndani bila musaada wowote. Walishikwa na kuletwa mpaka pwani katika wavu.


14/ Matendo ya Mitume 16: 19 

“Lakini wakati bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakakamata Paulo na Sila, wakawakokota hata sokoni mbele ya wakubwa wa mji.” 

Maandiko hapa ni kuhusu Paulo na Sila wakiwa hazarini sokoni. 

Walikuwa pasipo mwenye kuwasaidia wakakokotwa kwa nguvu. 

Pia tunaikuta tena katika Matendo ya Mitume 21: 30  

“Mji wote wakafazaika, watu wakakutanika mbiombio, wakakamata Paulo, wakamkokota inje ya hekalu; mara moja milango ilifungwa.” 

Maandiko hapa ni kuhusu Paulo na Sila wakiwa inje hazarani. 

Walimukokota Paulo inje ya hekalu. 

Walikuwa pasipo musaada toka kwa watu, wakikokotwa kwa nguvu. 

Ndani ya Matendo ya Mitume 21:30, imeandikwa kwamba: wakimukokota Paulo inje ya hekalu. 

Turudi kwa Andiko tuliloanza nalo: Yoane 12: 32  

“Nami kama nikinyanyuliwa juu ya dunia, nitakokota watu wote kwangu.”  

  Yawezekana kwamba, kati ya wanaadamu kuna wale wanaoweza kusema: Umbalimbali na yale, mimi sitaki kujongea kwake, sitaki nimuone uso kwa uso, sitaki nimupe hata muda wa kukutana nami. 

Bali, fahamu ndugu yangu ya kuwa kwa siku ile, hakuna mwenye atakuuliza lile unalolitaka, bali, wewe utasimama mbele ya kiti chake cha hukumu na kusimama mbele yake kwa kumujibu. 

Surulisho moja na jibu kwa swali hilo, mbele muda ingaliki bado, ni kukokotwa ndani ya Mapendo Yake kwa njia ya Neema yake kwa sasa, pahali pa kungojea kuonekana mbele Yake kwa hukumiwa, wakati itakuwa haiwezekani tena kwako kuweza kuokolewa. 


15/ Tuchunguze moja ya Maandiko yenye wanafurahia sana, iliyo katika 


Wafilipi 2: 9 – 11 

“Kwa hivi Mungu vilevile alimtukuza sana, na kumpa Jina lililo juu ya kila jina; 

Hata kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa, la vitu vya mbinguni na vya duniani, na chini ya dunia, na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” 

Neno “Kila” katika aya zote hizo yatoka kwa neno la Kigriki linalomaanisha “Yote”, sawa sawa na katika Maandiko mengine ya Biblia na ni hapo ndipo watu wa kilimwengu wote wanatoa mawazo ya kuhakikisha  kwamba Maandiko yale yanafundisha kwamba  kwa mwisho watu wote wataokolewa na hapo wanataja:  

Waroma 10: 9 

“Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua toka wafu, utaokolewa:” 

Bali wao hawataji: 


Wafilipi 2: 11 

“na kila ulimi ukiri ya juwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” 

Eti Andiko hili lafundisha kwamba kuna siku moja, kila ulimi utakiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana? Hapana hata kidogo, jibu ni HAPANA.  


Waroma 10: 9 – 10 

“Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua toka wafu, utaokolewa: 

Kwa maana kwa moyo mtu anaamini hata kupata haki; na kwa kinywa anakiri hata kupata wokovu.” 

Kukiri inatiwa pamoja na imani moyoni. 


Wafilipi 2: 9 – 11 

“Kwa hivi Mungu vilevile alimtukuza sana, na kumpa Jina lililo juu ya kila jina; 

Hata kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa, la vitu vya mbinguni na vya duniani, na chini ya dunia, na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.” 

Hapa haiambatane vile. 

Hapa inatiwa pamoja na jambo ambalo kila goti litapigwa, la watu wote bila ubaguzi. 

Tufahamu vizuri kwamba, wakati hali hiyo itatimilika, haitakuwa tena wakati wa kuamini moyoni mwetu ya kuwa Mungu alimfufua Kristo toka wafu, sababu, kwa wakati ule Ufufuko wake utakuwa wazi dhahiri. 

Andiko la Waroma 10: 9 – 10, yaonekana wazi kwamba ni shauri, pendekezo. 


Waroma 10: 9 – 10 

“Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua toka wafu, utaokolewa: 

Kwa maana kwa moyo mtu anaamini hata kupata haki; na kwa kinywa anakiri hata kupata wokovu.”  


Wafilipi 2: 9 – 11 

“Kwa hivi Mungu vilevile alimtukuza sana, na kumpa Jina lililo juu ya kila jina; 

Hata kwa Jina la Yesu kila goti litapigwa, la vitu vya mbinguni na vya duniani, na chini ya dunia, na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.”  

Amini sasa hivi Bwana Yesu, kama Bwana na Mwokozi wako, na utaokolewa. 

Kama unakataa ombi hili, kumbuka kwamba kufwatana na Maandiko ya Wafilipi 2: 9 - 11, upende ama usipopenda, siku moja itakuja ambalo utalazimishwa kumufahamu.  

Aya hii inatufundisha kugandamizwa ama kushushwa ya ulimwengu wote, 

bali halitufundishe ushirika wa ulimwengu wote. 

Mutatambuwa kwamba Mwenyezi Mungu alimupa Yesu Kristo Jina lililo juu ya majina yote. 

Ni Jina lenye litajaa duniani kwote, kama vile ninavyo amini, ni jina lenye munalolipenda. 

Jina hilo ni la ajabu sana. 

Jina nzuri kwa ulimi ya watu wote, nyimbo ya furaha sana kuliko. 

Naamini kwamba ni jina lenye ungelipendelea mtoto mchanga alitamke kwanza. 

Pendekezo lako ni kwamba mbele mtoto wako mchanga ajue kusema ama kutamka neno la kwanza, angelianza kutaja Jina Yesu Kristo, na pia kwa watu makamu, wazee, mbele watoe pumzi yao ya mwisho, ungelipendelea wataje jina la Yesu Kristo.  


16/ Goti na ulimi. 

Goti litapigwa mbele ya Kristo, hata magoti ya wa milioni ya watu wanaopotea, wakaidi wanao sengenya na kumuchekelea, vizazi vya laani wenye kucheza na Jina la Kristo bure, wote watamukiri kwamba Yeye ni Bwana. 

Kweli, Mungu anasema kwa wale watu wenye kiburi wenye wanakataa kupiga magoti mbele ya Yesu, Mungu atasema: Munapashwa piga magoti yenu mbele ya Jina la Yesu na ndimi zenu zinapashwa kumukiri, bali kwa wakati ule itakuwa jambo la kunyanyasa, la kutiishwa. 


17/ 1 Timoteo 2: 4 - 6  

“anayetaka watu wote waokolewe na kupata kujua sana yaliyo kweli.

Kwa sababu Mungu ni mmoja tu, na mpatanishi katikati ya Mungu na watu ni mmoja, yule mtu Kristo Yesu, ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote; utakaoshuhudiwa kwa wakati wake;” 

Kwa andiko hili wale watu wa zehebu ya kilimwengu wanasema kwamba: Kama Mungu anahitaji watu wote waokolewe na Yeye haitimize, ni kusema kama Yeye ayupo mahali pote, na Kristo alikufa kama mtu aliyechindwa. 

Masimi yao yanafanana kuwa sambamba lakini sivyo. 

Tulinganishe Maandiko haya na Maandiko yafwatao:  


Ezekieli 18: 20 -23 

“Nafsi inayofanya zambi itakufa, mwana hatabeba uovu wa baba, wala baba hatabeba uovu wa mwana; haki ya mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu ya mwovu utakuwa juu yake. 

Lakini kama mwovu akigeuka toka zambi zake zote ambazo alizitenda, na kuchunga sheria zangu zote, na kutenda hukumu na haki, hakika ataishi, hatakufa. 

Zambi zake zote ambazo alizifanya hazitakumbukwa juu yake, kwa haki ambayo aliitenda ataishi. 

Mimi ninafurahi kwa kufa kwa mwovu? 

Bwana MUNGU anasema; na si zaidi ageuke toka njia yake, na kuishi?” 

Kwa aya ya 23 anasema:  

Eti mimi ninafurahi kwa kufa kwa mwovu? HAPANA 

Bali, tunajuwa kwamba aya ya 20, inatuambia kwamba mwovu atakufa. 


18/ Tunapashwa kuchunguza kwa makini kabisa masemi ya 


1 Timoteo 2: 4 -6  

“anayetaka watu wote waokolewe na kupata kujua sana yaliyo kweli.

Kwa sababu Mungu ni mmoja tu, na mpatanishi katikati ya Mungu na watu ni mmoja, yule mtu Kristo Yesu, ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote; utakaoshuhudiwa kwa wakati wake;” 

  Maombi kwa wengine inafwatwa na musemwa unaosema kwamba Mungu anataka watu wote waokolewe, na kwamba Kristo alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya watu wote, kwa hiyo, wazo ni kwamba Mungu anahitaji watu wote waokolewe, kwa sababu Kristo alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote. 

Sisi tulio wake twapasa kuwa na nia hiyo na kutamani kuombea wengine. 

Nasi tunatamani watu wote waokolewe, lakini tunajuwa ya kwamba Mwenyezi Mungu hawezi kuokowa mtu asiyemjia kwa kupitiya njia ya Yesu Kristo. 


19/ Tuone sasa Maandiko mengine yenye wanapenda kuonesha. 


1 Timoteo 4: 10 

“Kwa sababu hii tunajitahabisha na kulaumiwa sana, kwa sababu tunatumainia Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, zaidi wa hawa wanaoamini.” 

Mungu ni Mwokozi wa watu wote, zaidi sana wa hawa wanaoamini. 

Ni huzuni sana kuona watu wa zehebu ya Kiulimwengu kufikia kuzania kwamba wanaweza kutumia Andiko hili kwa kuonesha kwamba watu wote wataokolewa. 

Mutatambuwa kwamba neno “mwokozi” yaweza kumaanisha “Mlinzi”: Yeye ni Mlinzi wa wote wanaoamini. Hii aimaanishi kazi ya Kristo kuhusu wokovu. 

Ni picha tu ya Mungu kama Muumbaji na Mlinzi wa watu wote. 

Katika Zaburi 36: 6 

“Haki yako ni kama milima ya Mungu; Hukumu yako ni vilindi vikubwa; 

Ee Bwana, unaokoa mtu na nyama.” 

Ni namna hivyo tu ndivyo afanyavyo. 

Kumbukeni asemavyo katika Matayo 5: 45 

“Mupate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni, sababu Yeye anaangazia jua lake waovu na wema, naye ananyeshea mvua wenye haki na wasio haki.” 

Zawadi yote nzuri na kamilifu inatoka kwake Mungu, na watu wote wanaoamini na wasioamini kwao wote pamoja Mungu ni mlinzi wa maisha yao wote.  

Ni yeye aliyeumba ulimwengu na kuweka nguvu zinazoongoza ulimwengu, siyo tu juu ya watu, lakini pia juu ya wanyama, na zaidi sana juu ya wale wanaoamini. 

Anatushurulikia kwa sababu vitu vyote vinatumika pamoja juu ya mema yetu. 


20/ Muniruhusu niwape mfano wa jambo Mwenyezi Mungu alilolifanya juu ya Mtume Paulo. 


2 Wakorinto 11: 32 – 33 

“Katika Damasiki mtawala wa mfalme Areta alilinda mji wa Wadamasiki apate kunikamata: 

Na kutoka dirisha nilishushwa kwa ukuta ndani ya kitunga, na nikaponyoka toka mikono yake.” 

Hapa kwa namna ya upekee, Mwenyezi Mungu Mwenyewe alikuwa mlinzi wa Paulo. 


21/ Tuchunguze sasa Maandiko mengine moja moja. 

Eti, Maandiko yale yanatuambia kwamba kuna siku moja watu wote wataokolewa?  

Wafilipi 3: 19 

“mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao ni haya yao, wanaofikiri maneno ya dunia.” 

Tambueni yanayosemwa hapa: Wao ni adui za Msalaba wa Kristo, na nini iliyo mwisho wa wale walio maadui za Musalaba wa Kristo? 

  Ni upotevu, ni uharibifu, ni laana. 

Eti jambo hili linaambatana na mawazo ya kwamba mwisho wao ni wokovu? Hapana, mwisho wao ni upotevu, ni laana.  


22/ Tupime kusonga mbele na mawazo haya: 

Kama katika Waroma 8: 33 tunaulizwa:  

“Ni nani atakayeshitaki wachaguliwa wa Mungu?” 

Kama ingelikuwa kwamba mawazo inayosemwa na watu wa zehebu ya kilimwengu ni ya kweli, tungelipashwa kusoma namna hii: 

Ni nani atakayeshitaki mtu yeyote ule? Sababu watu wote wataokolewa, Hapana hii Andiko ingeligeuka isiyo na maana. 

Tutwae sasa Waroma 8: 28 

“Na tunajua maneno yote yanafanya kazi pamoja kuwapatia mema wale wanaopenda Mungu, kwa wale walioitwa kwa kusudi lake.” 

Sababu gani haikusemwa: 

Mwenyezi Mungu anafanya maneno yote yafanye kazi pamoja kuwapatia mema watu wote? 

Kwa sababu gani ni kwa wale wanao mpenda Mungu peke yake? 


23/ Hata tunafikia kiwango wanapowaza kwamba hata Shetani siku moja ataokolewa. 

Mapepo wachafu wote wataokolewa, hii ni mafundisho ya upumbafu. 

Tuchunguze tena Maandiko yafwatao:  


2 Wakorinto 11: 13 – 15 

“Maana hawa ni mitume ya uongo, wenye kutenda kazi kwa hila, wakijigeuza wenyewe kuwa kama mitume ya Kristo. 

Wala si ajabu; kwa sababu Shetani mwenyewe anajigeuza awe malaika ya nuru. 

Basi si neno kubwa kama watumishi wake vilevile wanajigeuza wawe watumishi wa haki; mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.” 

Tambueni kwamba inasemwa hapa ya kwamba: 

Wenye mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.  

Hawastahili wokovu. 

Mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. 


AMINA


N°Ref: 11/11/1962/ 252 - WILL ALL MEN BE SAVED /9/6/2021