Wednesday, April 29, 2020

NEEMA NI JIBU / GRACE IS THE ANSWER

Lake Kivu at sunset








     NEEMA NI JIBU
     321 - GRACE IS THE ANSWER
     December 28, 1976 
     Pastor Henry F. Kulp 




Waefeso 2: 7 - 10 
“Hata katika nyakati za kuja aoneshe wingi wa kupita kiasi wa neema yake kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu; 
Kwa maana mumeokolewa kwa neema kwa njia ya Imani, wala neno hili halikutoka ndani yenu wenyewe, ni zawadi ya Mungu, 
Si kwa matendo, asiwe mutu atakayejisifu. 
Maana sisi ni kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu ili tutende mema Mungu aliyotengeneza mbele ili tutembee ndani yao.” 
Hapa tunapata maandiko matamu na marembo sana. 
Wengi wenu wanafahamu kwa moyo sura mbili ya hii maandiko na yawezekana  sura ine.  Kwa binafsi  ningewasihi mushike na kufahamu kwa moyo,  sura hizo zote ine na mupate kuvumbuwa ukweli  mukubwa sana na wa muhimu wenye  kuonyeshwa hapa. 

1/ Mwenyezi Mungu ana miradi ama mipango yake inayotendeka si kwa kubahatisha. 
Mungu ni Mukamilifu kweli, na anatenda kazi zake zote na kupanga miradi yake yote  katika ukamilifu. 

2/ Inatupasa  kufahamu ya kuwa maisha ya mwamini ina  sehemu kubwa tatu: 
a. Wokovu 
b. Maisha ya hapa chini duniani mbele ya kutoweka ama kunyakuliwa. 
c. Umilele, wakati yuko pamoja na Bwana na Mwokozi wetu. 
Aya ya saba inazungumuza juu ya sehemu hii ya tatu, inayohusu  maisha ya milele ya mwamini. 
Shairi la nane(8) , na la kenda(9), inahusu sehemu ya kwanza yaani Wokovu,  kutoka kwenye mauti na kuingia uzima, kutoka kuwa mwana wa shetani na kugeuka kuwa mwana wa Mungu. 
Aya ya kumi ni sehemu ya pili, yaani maisha yetu hapa duniani kiisha wakovu, mbele ya kuhamishwa kwetu ama kunyakuliwa kwetu.
Tuchunguze sasa sehemu hizo tatu na tuone ujumbe gani Mwenyezi Mungu anapenda tufahamu. 

3/ Aya ya saba(7), hata katika nyakati za kuja. 
Hii inakuwa msemwa unaofwata ungine na kutuonesha kwamba  kuna jambo Mungu atatutendea  katika nyakati za kuja. 
KATIKA NYAKATI ZINAZO KUJA MOJA NYUMA YA NYINGINE. 
Inamaanisha katika umilele unaokuja, Mwenyezi Mungu atatutendea  jambo fulani. 

4/ ILI AONYESHE 
Hii ni neno maalum katika kigriki N-DIKE-NEW-ME na inamaanisha kuonyesha, kutambulisha, kuhakikisha kwa wazi. 
 ILI KWA KUONYESHA KWA KUHAKIKISHA KWA WAZI. 

5/ Ni nini Mwenyezi Mungu atakayo tuonesha kwa wazi? 
Wingi wa kupita kiasi wa neema yake kwa wema wake. 
Neno “ wa kupita kiasi”  ni HOOP – PEAR – BAL – O. 
Balo,  inamaanisha kutupa huko mbele na HOOP inamaanisha kupita kiasi na hapa inamaanisha nzuri sana kupita kiasi, nzuri sana zaidi na inasemwa kwa wakati wa sasa. 
Inamaanisha kwamba Mungu ataendelea kuitimiza kwa milele na milele. 
Ona raha za nyakati zetu za kuja. 
Utajiri sana, Samani kubwa kupita kiasi ni hii atatuonesha, samani kubwa zaidi ya wingi wa kupita kiasi wa wema wa Neema yake. 
Waroma 5: 20  
  “Lakini sheria iliingia, ili zambi ziwe kubwa sana; lakini pahali zambi zilipozidi, neema ilizidi zaidi sana:” 

6/ Namna gani kutofautisha na kujuwa umbalimbali kati ya hayo na namna anavyotuonesha  Neema kwa sasa? 
Kwa siku za leo, tumeokolewa kwa neema na tunakingwa na kuchungwa kwa neema. 
Lakini kwa leo, haiwezekane Mungu atuoneshe wingi wa kupita kiasi wa neema yake kwa wema, sababu tungali tukivaa mutu wetu wa zamani. 
Ni kwa hiyo, kuna wakati Mungu anaruhusu mateso yatufikie, yeye anatufunza na kutuhimiza, kuturekibisha, na mara kwa mara anaruhusu tupate mibaraka katika maisha yetu. 
Katika nyakati itakayo kuja, katika maisha ya umilele, utu wa zamani utaondoshwa na Mungu atatufurika na mibaraka, mateso hayatakuweko, hatutarekibishwa tena. Tuna nyakati za kuja za Baraka sana. 
Yote tunayoishi leo ni maonjo tu kidogokidogo ya hizo mibaraka. 

7/ Ingelikuwa kwamba Mwenyezi Mungu aliruhusu tuishi tu katika Baraka, sisi hatungeliwezekana, tungelijazwa na kiburi, tungelikuwa na uchoyo kiasi na tungelitamani kujisifu pahali pa kurudishia Mwenyezi Mungu Sifa. 


8/ Maana ya Neema ni vyote kwa bure  
Mara ngapi Neema iko ndani ya wingi wa kupita Neema kuzidi sana? 
Waroma 5: 20 
“Lakini sheria iliingia, ili zambi ziwe kubwa sana; lakini pahali zambi zilipozidi, neema ilizidi zaidi sana:” 
Katika hii aya tuna kipimo cha kuzidi sana cha Neema. 
Ni kupita sana zaidi hiyo tunayoweza kufikili. Mwenyezi Mungu atatufunulia hayo katika nyakati za umilele zinazokuja. 

9/ KATIKA WEMA 
Wema ni CRAY – STOW –TACE ni hii inamaanisha Ukaribishaji. 
Ni Mwenyezi Mungu alie Mukaribishaji Mkamilifu. 
Tukamate mfano wa baba mmoja aliye na mwana wake mume asiye kuwa kwa nafasi anapohitajika kuwa kwa wakati, anayekuwa na tabia ya kutenda maovu mengi hata baba yake hana ile wakati wa kumuonesha ukaribishaji wake, sababu kila wakati yuko nafikilijuu ya namna gani kuhazibu mtoto, kumurekibisha, lakini nyakati itakuja yenye huyu mwana ataamua kuachana na maisha ile mbaya na kwa saa hiyo baba ataanza kumukaribisha. 
Ni huu mwana njo alikuwa akizuiza wema wa baba yake. 
Katika YESU KRISTO haya yote ni kweli sababu sisi tunaunganishwa na KRISTO. 

10/ Aya ya nane(8), ya kenda(9) inatupeleka kwa sehemu ya kwanza. 
TUMEOKOLEWA KWA NEEMA KWA NJIA YA IMANI  
Katika kigriki, maneno haya hameandikwa katika nyakati inayoonesha kwamba tendo inazidi tu kuendelea. 
Ni tendo iliyoanza kwa ziku zilizo pita na yenye inaendelea katika nyakati na siku zitakazokuja. 
NI MUSALABA. 

11/ Kwa njia ya IMANI   
Hii njo vifaa ya Wokovu. 
IMANI na NEEMA njo vitu muhimu sana juu ya Wokovu. 
NEEMA ni mchango  kutoka kwa Mungu 
IMANI ni mchango kutoka kwa mwanadamu. 
Unacho lazimishwa kufanya ni kuamini tu na hakuna kustahili yoyote inayokuja kwa kuamini. 
Ni zawadi ya MUNGU. 
Imeandikwa waziwazi na kusomwa waziwazi: 
Wala neno hili halikutoka ndani yenu wenyewe. 
Neno hili, ni neno lisilo na tegemeo ama upendeleo, inaweza tumikishwa ngambo zote, bila kubadili  aina ya Neema, sawa vile  aina ya Imani na haibadirishe kitu kwa Wokovu. 

12/ Ni zawadi ya Mungu 

13/ Si kwa matendo   
Hii inamanisha nini? 
Hii inamaana ya kusema kwamba, si kwa tabia nzuri ama kazi nzuri ya kimutu. 
Inatupaswa kufahamu kwamba tungali tunavaa utu wetu wa zamani. Na siyo zambi tu njo mutu wa zamani anaweza tenda, ila  mutu wa zamani anaweza vilevile kutenda matendo ama tabia nzuri za kimutu. 
Lakini yatupasa vile vile kufahamu kwamba tabia nzuri za mwanadamu ni kufa. 
Wahebrania 6: 1  
“Kwa sababu ile, tukiacha mafundisho ya kwanza ya Kristo, tuendelee hata utimilifu; tusiweke tena msingi wa kutubu kwa kazi za kufa, na ya Imani kwa Mungu.” 
Matendo yote mazuri na tabia yote muzuri ya mwanadamu ni matendo ya kufa. 
Tabia hizi ni za kufa kama tukilinganisha na kuwaza juu ya Mungu, lakini sivyo vile kama maelekezo ni kwa mutu. 
Na hapo yafaa tutambuwe kwamba matendo mazuri ya mwanadamu, ni matendo ya kufa mbele ya macho ya Mungu tena matendo yale hayakubaliwe na Mwenyezi Mungu. 
Isaya 64: 6 
“Lakini sisi sote tumekuwa kama kitu kichafu, na haki zetu zote ni kama vitambaa vya kupasukapasuka vya taka; sisi sote tunakauka kama jani, na maovu  yetu yametuondoa, kama upepo unavyoondoa,” 
Tabia zote nzuri tunazo na matendo yote mazuri tufanyayo ni kama taka. 

14/ Tabia na Matendo nzuri ya mwanadamu haiwezi kuokowa 
Waroma 11: 6 
“Lakini ikiwa kwa neema yake, haiko kwa matendo tena, au neema isingekuwa neema; na ikawa kwa matendo, haiko neema tena; au matendo yasingekuwa matendo.”  
2 Timoteo 1: 9 
“ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, lakini kwa kadiri ya kusudi lake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa katika Kristo Yesu mbele ya nyakati za zamani,”  
Tito 3: 5, 7 
“Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyafanya lakini kwa rehema yake alituokoa, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa mpya na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 
7. tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa wariti kwa tumaini la uzima wa milele.” 

15/ Tuchunguze hapa utu wa zamani na tabia na matendo mazuri ya mwanadamu. 
Wanadamu waliumbwa bila kuwa na zambi ya asili, ni kwa sababu hiyo walikuwa na ufahamu juu ya tabia na matendo mema. 
Lakini tangia siku mwanadamu alianguka, alipokea ule utu wa zambi, ule utu wa zamani na tendo la kwanza lenye mwanadamu alilolifanya kiisha kuanguka ni tendo nzuri ni hiyo Kazi ya kujijengea nguo ya majani. 
Kazi ya mwanadamu aliyo ifanya ya kwanza baada ya kuanguka, kazi hiyo haikuwa ya zambi lakini kazi nzuri ya kufunika uchi ama utupu wake.  

16/ Asiwe mutu atakaye jisifu 
Kujisifu inamaanisha nini? 
Ni kupata kusudi ama tendo katika maisha yako,  itakaokuonesha wewe kama mutu mwema. 
Ni hiyo mwanadamu anajikaza daima kutimiza  katika dini mbalimbali. 
1 Wakorinto 1: 30, 31 
“Lakini kwa yeye ninyi ni katika Yesu, aliyefanyizwa na Mungu kuwa kwetu akili, na haki, na utakaso na ukombozi; 
Hata sawasawa ilivyoandikwa: Yeye mwenye kujisifu, ajisifu katika Bwana.” 
1 Wakorinto 4: 7 
“Basi ni nani ambaye anakufanya kuwa mbalimbali? 
Nawe una kitu gani usichopokea? Lakini kama ulikipokea, kwa nini unajisifu sawasawa hukupokea?  

AMINA 


N°Ref: 12/26/1976 / 321 - GRACE IS THE ANSWER / 2020 

No comments:

Post a Comment