Photo by B Smith from the patio
MKAKATI WA MALAIKA ALIYEANGUKA
THE STRATEGY OF THE MOCK ANGEL
January 1, 1961
Pastor Henry F. KULP
Waefeso 6: 10
“Basi kwa kumaliza, muzidi kuwa hodari katika Bwana, na katika uwezo wake.” Tulikuwa tukizungumuza kuhusu vita kubwa ama mapambano yanayo mkumba mukristo.
Yampasa yeye ndiye awe mwenye kushambulia.
Ni yeye anayepaswa kuongoza na kuleta maelekeo.
Kwa kweli adui wake ni Shetani na mapepo wake wachafu.
Mwenye kustahili kupambana na Shetani katika vita hivi ni mukristo aliye komaa. Hatuwatumi watoto wachanga kwenye vita.
Hatuwatumi vilevile watoto wadogo kwenda kwenye vita, hata mbele ya macho ya Mungu ni hivyo, Mwenyezi Mungu hatarajie watoto wachanga kwenda kupigana vita na shetani, kwa maana, wao hawajuwi ni wapi kuanzia, kwa hiyo yatupasa tukomae kiroho, ili tufike kiwango cha kupambana katika vita na kuwa washindaji.
1/ Shabaa ya Shetani si kwamba tupoteze wokovu wetu.
Shetani anapenda akuibe vifaa vya taji utakayovikwa.
Yeye hafurahie wewe kupata zawabu kulingana na maisha yako ya kikristo.
Maisha ya wakristo wengi yanakuwa na uzembe kuhusu mapambano haya. Kiini yao siyo kujipanga zidi ya kuwa tayari katika mapambano haya.
Wamezarau vita hivi, kwao wamesema wameokolewa na hiyo yatosha kwao, na hii inaonesha lengo ya maisha yao ya kikristo ni ya aina gani.Wamezarau vita hivi, kwao wamesema wameokolewa na hiyo yatosha kwao, na hii inaonesha lengo ya maisha yao ya kikristo ni ya aina gani.
2/ Tujihazari kufahamu nini iliyo chanzo cha nguvu za watakatifu. Jambo hili ni la maana kweli:
Kwa kuanza mapambano katika vita hivi, yatupasa tuwe wenye nguvu katika Bwana, kuvaa nguvu za Uwezo wake.Kwa kuanza mapambano katika vita hivi, yatupasa tuwe wenye nguvu katika Bwana, kuvaa nguvu za Uwezo wake.
Neno “kuwa hodari” inamaanisha kuvaa uwezo ama kufanywa kuwa mwenye uwezo. Ni mtu gani anayetuomba tuwe hodari katika Bwana?
Wakati wowote kama unapata mashauri toka mtu fulani, yafaa kweli kujuwa ni nani anayekushauria.
Ni mtu wa aina gani na tabia zake ni gani?
Yeye anaujuzi kweli wa mambo anayokushauria?
Katika ulimwengu huu, ni wengi wanaopenda kupana mashauri hata kwa jambo wasiloelewa vizuri, hawafahamu ni nini wanaosema.
Wanapenda wakushauriye kuhusu namna ya kuongoza jamaa lako, namna gani kulea watoto wako, bima gani kununua kwa niaba ya vifaa vyako, gari gani yafaa kununua, wapi kuishi na mara nyingi wao wenyewe hawakufaulu, sasa wao watakushauri namna gani?
Lakini, tutizame sasa, mtu huyu Mtume Paulo ni nani? Yeye anayetuhimidi tuwe hodari katika Bwana?
Eti yeye alikuwa myonge ama goigoi ama mzaifu? Mimi nina uhakika kama sivyo.
Yeye hakuwa mtu wa hivi hivi.
Paulo alikuwa mtu aliyefahamu maana ya kuwa hodari katika Bwana.
Yeye alikuwa tiyari kwa kupambana vita hivi, na alifahamu kwa uhakika maana ya kuvumilia katika Yesu Kristo.
Yeye alipigwa mawe, alisongwa na maumivu ya vidonda vikali, alifungwa minyororo, alitupwa katika gereza la shimo la chini, lakini alidumu katika mapambano. Wakati alikuwa akihimiza wakristo wawe hodari katika Bwana, yeye mwenyewe alikuwa akipitia katika shida na uchungu mkali.Paulo alikuwa mtu aliyefahamu maana ya kuwa hodari katika Bwana.
Yeye alikuwa tiyari kwa kupambana vita hivi, na alifahamu kwa uhakika maana ya kuvumilia katika Yesu Kristo.
Yeye alipigwa mawe, alisongwa na maumivu ya vidonda vikali, alifungwa minyororo, alitupwa katika gereza la shimo la chini, lakini alidumu katika mapambano. Wakati alikuwa akihimiza wakristo wawe hodari katika Bwana, yeye mwenyewe alikuwa akipitia katika shida na uchungu mkali.
3/ Wagalatia 6: 17
“Tangu sasa mtu asinisumbushe, kwa maana ninachukua katika mwili wangu
chapa zake Bwana Yesu.” Mtume Paulo asema hivi:
Tangu sasa mtu asinisumbushe.
Hawa watu wa Galatia waliingiliwa na walimu waliowafundisha kwamba mtu yule Paulo si Mtumishi wa Yesu Kristo, yeye siye Mtume, kwa nini kumusikiliza?
Paulo aliwaambia: Munafahamu ya kwamba mimi ninachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu Kristo.
Tufahamu hapa kwamba alitia mkazo akitumia neno “mimi” kwa kujilinganisha na wale walimu wa kiyuda.
Aliwafahamisha ya kwamba, hata kwa wakati anapozungumuza nao yeye anazo chapa za Yesu Kristo katika mwili wake.
Chapa hizo ni gani?
Sababu gani tayari zimewekwa hapa?
Ni vidonda na makovu mabichi, na namna mzuri ya kutafsiri neno “chapa” ni kwa kutumia neno “kovu” na ni hapo tunapopata neno “Unyanyapaa” katika Swahili. Yeye alikuwa kweli na alama maalum.
Kulikuwa makovu na vindonda vya kuumia vya kila nyakati.
Yeye alipigwa mawe, alikuwa na chapa ya vidonda vya kupigwa fimbo, alifungwa minyororo, hayo vidonda, makovu na alama maalum yalionekana wazi mwilini mwake na yalimuhofu sana.
Alama hizo zilikuwa wazi na mbichi mwilini mwake.
Kwa kweli mimi ninaweza kubali mashauri yatokao kwa mtu kama yeye.
Wakati anaponiambia niwe hodari katika Bwana, najuwa kwamba yeye mwenyewe ajuwa maana ya kuwa hodari katika Bwana, pia hufahamu kwamba yawezekana kuwa na hali hiyo ya uhodari.
Yeye ni mtu analiyefaa kupana shauri za namna sawa.
4/ Mtu aliyetuhimidi tuwe hodari, yeye mwenyewe alikuwa hodari.
Wakati alipokuwa akiandika Maandiko haya, alikuwa akipatikana katika gereza la chimo la chini iliyopatikana kwenye makao ya kifalme.
Bali, huko gerezani, chini ya udongo, yeye alidumu tu akimuhudumia Bwana Yesu Kristo, alikuwa akisonga mbele kwa kupiga vita vema akijitahidi ili apate taji lake. Kuna taji inayoandaliwa kwa yoyote yule atakaye leta nafsi kwa Yesu Kristo.
Yeye alipata taji nyingi wakati bado alipokuwa angali katika gereza ya shimo la chini, yeye alikuwa akishuhudia Yesu Kristo kwa kila mtu aliyekutana naye ndani ya gereza.Wakati alipokuwa akiandika Maandiko haya, alikuwa akipatikana katika gereza la chimo la chini iliyopatikana kwenye makao ya kifalme.
Bali, huko gerezani, chini ya udongo, yeye alidumu tu akimuhudumia Bwana Yesu Kristo, alikuwa akisonga mbele kwa kupiga vita vema akijitahidi ili apate taji lake. Kuna taji inayoandaliwa kwa yoyote yule atakaye leta nafsi kwa Yesu Kristo.
Yeye alipata taji nyingi wakati bado alipokuwa angali katika gereza ya shimo la chini, yeye alikuwa akishuhudia Yesu Kristo kwa kila mtu aliyekutana naye ndani ya gereza.
Wafilipi 4: 22
“Watakatifu wote wanawasalimu ninyi, zaidi wale walio nyumbani mwa Kaisari”. Mtume Paulo anahakikisha eneo gani? Wale walio nyumbani mwa Kaisari.
Kumbukeni kwamba Mtume Paulo alikuwa katika gereza la chini ya udongo kwa nyumba ya Kaisari, na kweli ni vigumu kukubali kwamba ni katika mahali kama hapo ndipo angaliweza kusubutu kufungua kinywa chake kwa kuzidi tena kushuhudia mbele ya watu wengine wa nyumba ya Kaisari, lakini kwa kweli yeye alifanya hivyo.
Kwa kweli Neno aliloshuhudia liligusa na kukomboa nafsi za wafanyakazi wa ndani ya nyumba, waaskari, na hata vilevile wamoja wa Wakubwa wa waaskari, na yawezakana, humo ndani waliunda hata kanisa ndogo, ama muungano wa waamini waliokuwa nyumbani mwa Kaisari.
Yeye alipambana vitani hadi mwisho.
Kweli ni wajibu wangu kumusikiliza mtu kama huyo.
NINAWEZA KUKOKOTA KITI CHANGU NA KUKARIBISHA SIKIO LANGU ILI NISIKILIZE SIRI YA HIYO NGUVU.
5/ Kwa kweli, ombi la kutuhimiza tuwe hodari katika Bwana lafwatana na lingine linalotuomba kwamba:
Tuvae silaha zote za Mungu, tupate kuweza kupinga hila zote za Shetani.Tuvae silaha zote za Mungu, tupate kuweza kupinga hila zote za Shetani. Waefeso 6: 11
“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kupinga hila zote za Shetani.” Fahameni kwamba hapa kuna mupinganizi.
Mupinganizi wetu ametajwa, yeye ni Shetani na silaha zake zinajulikana kwamba ni hila.
Tujifunze kwa makini mpinganizi wetu, ili tufahamu namna gani tupasalo kupambana vitani humo.
Mara nyingi tunayo mawazo ya kuzania kwamba vita tunavyo ni vya mwili na damu, dada zetu na kaka zetu katika nyumba, rafiki katika jamii, majirani katika mtaa mpana, washirika wetu katika biashara, huyo mtu anayetuletea migorogoro na shida nyingi katika nyumba.
Tufahamu sana kwamba vita vyetu si vya damu na mwili.
Kweli mwili na damu yaweza kutupitisha kwenye majaribu makali sana, wajirani vilevile wanaweza kuchekelea hali yetu.
Hata mara nyingine wapendwa wetu katika jamaa, waweza kuwa na mume ama muke anayechukia upendo wako kwa Bwana Yesu Kristo na namna unavyomuzingatia. Waweza kuwa na watoto wenye hawaheshimu lile unalowaamuru watende, na vivi hivi. Bali mapambano tunayo maishani mwetu, si hiyo. Kwa kweli.
6/ Tufahamu kwa makini kabisa kwamba hatushindani na damu na mwili, ila tunashindana na Shetani na majeshi ya wafuasi wake mapepo wabaya.
Taswira na wazo tunayo hapa ni magonvi ya kupambana mwili kwa mwili, tukiwa mikono mitupu.Taswira na wazo tunayo hapa ni magonvi ya kupambana mwili kwa mwili, tukiwa mikono mitupu.
Wagriki walifahamu kabisa kabisa wakati Mtume Paulo alipotumia neno kushindana. Ilikuwa vita na ugonvi mwili kwa mwili, kila mmoja akitumia nguvu zake zote ili amugandamize mwenzewe na kumutupa chini.
Katika mashindano haya, mshindi anagandamiza mwenzake akimufinyanga kwa udongo na, katika aina ya ugonvi huu wa kigriki, mecho ya yule aliyeshindwa yaweza kutobolewa na kuwa na bahati mbaya ya kubaki kipofu kwa maisha yake yote, naamini kwamba kwa mwangaza wa picha hii munafahamu namna gani wakristo wa Efeso walitambuwa vita gani Mtume Paulo alionesha wakati aliandika neno kushindana.
Siyo jambo la mizaa, siyo mambo ya hivihivi, lakini ni vita ya hofu kubwa.
7/ Tukifahamu jambo hili vichwani mwetu, tusome sasa aya ya kumi na moja (11): Ya tuambia kwamba tuvae silaha zote za Mungu, ili tupate kuweza kusimama juu imara, hapana kutupwa chini na kuanguka, tusigandamizwe chini kwa udongo, lakini tuweze kusimama imara tukishindana na nguvu za hila za Shetani.
Neno hila, inamaanisha namna ya kutenda ya uerevu na ujuzi maalum, ama waweza kutumia neno Mkakati.
Shetani atumia mkakati ya ujuzi maalum kwa kushindana nasi.
Ingekuwa raisi sana, sawa michezo ya kitoto, kama Shetani angaliweza kujitokeza mbele yetu na kusema: Amjambo, mimi ni Shetani na vivi hivi.
Mimi ni mjumbe wa kazi za giza toka kwa bwana wangu Diabolo, na mimi nitahitaji wewe ukubali kuingia katika jambo hili lenye litakuletea mateso, hofu na shida
kubwa, umasikini na kumukana Mwokozi wako, na kuharibu hata ushuhuda wako, ni wajibu wako kunisikiliza tu ili mambo haya yote yatimie.
Kwa upesi sana tungejibu: Uwe mbali sana nami ewe Shetani, sitaki hata jambo moja toka kwako, na sina uhusiano nawe, ondoka.
Bali, shetani hatumike namna sawa.
Majeshi wake pepo wabaya hawatumie uendeshaji wa namna sawa.
Tunapata mfano muzuri katika Kitabu cha Yosua sawa sawa na namna nilihitaji tufahamu.
Kumbukeni namna tulivyowaambia kwamba Kitabu ya Yosua katika Agano la Kale inalinganishwa na Kitabu ya Waefeso katika Agano Jipya.
8/ Mwenyezi Mungu alimuhimidi Yosua atambuke mto Yordani, na kwamba ni kwa pwani la ngambo ndipo atakapokuta Inchi yenye Mungu alimupa, mahali kunako Taifa saba ya wa Kanana.
Ilikuwa mataifa yenye kujaa ukorofi, uchafu wote, yenye laana na kuabudu miungu, na Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba wasiwe na uhusiliano wowote na taifa zile, wasioane nao, bali wawaangamize, wawaangamize wote bila kubaki hata mmoja wao. Maagizo yalikuwa waziwazi na Yosua na Taifa nzima walikuwa wakiyaheshimu sawa sawa na namna Mwenyezi Mungu alivyowaahidi, hadi hapo.Ilikuwa mataifa yenye kujaa ukorofi, uchafu wote, yenye laana na kuabudu miungu, na Mwenyezi Mungu aliwaambia kwamba wasiwe na uhusiliano wowote na taifa zile, wasioane nao, bali wawaangamize, wawaangamize wote bila kubaki hata mmoja wao. Maagizo yalikuwa waziwazi na Yosua na Taifa nzima walikuwa wakiyaheshimu sawa sawa na namna Mwenyezi Mungu alivyowaahidi, hadi hapo.
Siku moja kulikuwa umati wa wageni wamoja waliokuwa wakivikwa nguo za kuchakaachakaa na zenyi tayari zimekwisha pasukapasuka, watu hawa walikuwa wakitembea polepole kwa barabara kubwa.
Walikuwa wakivaa viatu vya kambakamba kwenye miguu yao na mikononi mwao walikuwa na ndaa ndogo zikiwemo mikati yenye imekwisha kuozana walikuwa pia na vibuyu vya maji vilivyojengwa na ngozi ya mbuzi vyenye tayari vimekwisha pia kuchakaa na kutobokatoboka, na vikavu.
Kiisha wapelelezi wa Yosua wakakwenda kukutana nao na kuwauliza: wao ni wanani na wanahitaji nini?
Waliwajibu ya kwamba wanahitaji kumwona Akida mkuu wao.
Na wakati walipopelekwa mbele ya uso wa Yosua, Yosua akawauliza: Munataka tuwafanyie nini pia munatoka wapi?
Walijibu kwamba:
Kama vile hali ya mavazi yetu yaonesha, sisi tunatoka kwa muji wa mbali sana, vazi zetu zilikuwa mpya kweli siku tuliacha nyumba zetu na kuanza safari, mwaweza kutambuwa kwamba tulifanya safari ndefu.
Viato tunavyo kwa miguu yetu, tuliviuza toka muuzaji mmoja siku tuliyoondoka na kuanza safari yetu, mwaona sasa katika hali gani vinakuwa leo, vikichakaa na kupasukapasuka.
Na mikate haya yalikuwa yakitoka kwa tanuri, lakini sasa yameoza.
Sisi tunatoka safari ya mbali sana tukitembea, sababu tulisikia habari yenu toka mbali, namna gani huyo Mungu yuko pamoja nanyi, kwa hiyo tulitamani tufanya ushirikiano pamoja nanyi.
Eti, mwakubali tuwe marafiki?
Ni jambo la heshima kwetu kuungana pamoja nanyi, kwa hiyo twawaomba tafazali, tufanye patano la ushirikiano pamoja nanyi.
Yosua akasema, kweli hii ni jambo la kushangaza.
Yawezekana je, kufwatana na eneo kubwa hili la jangwa linalotutenga, nyinyi musikie habari zetu namna gani?
Wakajibu: Oh habari zenu zilitambaa na kuenea dunia nzima.
Tulisikia namna gani muliingia na ushindi wakati mulipofika katika mahali hii, namna gani Jeriko na Ayi zilianguka mikononi mwenu, bali kwa sasa tafazali tuungane na tufanye patano la ushirikiano.
Ni namna hiyo ndiyo twasoma kwamba watu wale walifanya mapatano nao, na bila kumuuliza Mwenyezi Mungu mashauri.
Yosua 9: 14 - 16
“Watu wakachukua chakula chao na hawakuuliza shauri kwa kinywa cha BWANA. Yosua akafanya salama nao, akafanya mapatano nao ili kuwaacha hai, wakubwa wa makutano wakawaapia.
Ilikuwa kwa mwisho wa siku tatu nyuma ya kufanya mapatano nao, wakasikia ya kama walikuwa jirani za karibu nao, wakakaa katikati yao.”
Kwa hiyo walidanganywa na hila za mkakati za wa Gabaoni, baada ya kufanya mapatano nao kiisha siku moja ama miwili, wakati haikuwa tena raisi kuyavunja ni hapo sasa ndipo walitambua kwamba watu wale walikuja toka mungini iliyo jirani na kwahiyo walipenda kwa shali ama kwa mema waungane na kufanya salama nao ili waponeshe nafsi zao na kubaki hai.
Hiyo ndiyo picha ya matumikio ya Shetani na malaika wake pepo wabaya wanapojiingiza katikati ya wana wa Mungu.
Wanatumia mbino za wajuzi, hawajitokeze namna wengi wanavyozania.
9/ Watu wanaweza sema kwamba mtu fulani iko anakwenda kuona mashetani. Wao hawatambui kwamba shetani hana lakufanya na maneno ya namna sawa. Siyo kosa lake.
Sasa Shetani anakuja namna gani?Sasa Shetani anakuja namna gani?
Tunayo zoezi ya kutumia Maandiko Matakatifu bali, mpaka hapo, watu hawana ufahamu.
2 Wakorinto 11: 3
“Lakini ninaogopa, ya kwamba sawasawa nyoka alivyodanganya Hawa kwa hila yake, mawazo yenu yataharibiwa, na mutaacha weupe wa moyo na usafi katika Kristo.” Hapa Mtume Paulo anasema ya kwamba:
Sawasawa namna mawazo yenu yanaharibiwa na munaacha weupe wa moyo na usafi katika Kristo, na kwa kweli anayefanya hivi ni Shetani, Diabulo.
Weupe wa moyo na usafi katika Kristo.
Ni waamini wengi wasioshikamana na weupe wa moyo na usafi katika Kristo. Wanapenda kuonesha kwamba ni vigumu sana kuishi katika hali hiyo.
Kwa kweli ingekuwa faida, kwa musaada wa Roho Mtakatifu kufikia kutimiza lengo la kuishi ndani ya hali hiyo.
Kwa kweli ingelikuwa heri kuipambanisha na mambo mbalimbali ya maisha ya kila siku. Ingelikuwa heri kuwa na hamu ya hali hiyo.
Ingelikuwa heri kuwa na tabia ya maisha mazuri, pahali pa kusadiki Yesu Kristo kwa Imani tu, ila kujitahidi siku kwa siku kumtazamia tu Bwana Yesu Kristo, roho ikijaa na Neno la Mungu.
Siyo mshangazo kuona Shetani akiwashinda wakristo wa desturi akiwaangusha na mbino za hila zake.
Anafanya hivyo kwa njia gani?
Shika jambo hili kwa makini sana: Kwa njia ya nia ya mawazo, Shetani hutumia njia hii ya mawazo, ni lazima na muhimu kufahamu jambo hili.
Shetani anatumikisha mafikili, ama mawazo ya mwamini, mapambano haya ya ugonvi wa mwili kwa mwili ufanyika katika nia ama mafikili.
10/ Tuchunguze sasa namna Shetani anavyotumika:
2 Wakorinto 11: 13 – 14
“Maana hawa ni mitume ya uwongo, wenye kutenda kazi kwa hila, wakijigeuza wenyewe kuwa kama mitume ya Kristo.
Wala si ajabu; kwa sababu Shetani mwenyewe anajigeuza awe malaika ya nuru.” Anajigeuza mwenyewe awe malaika ya nuru. Yeye haje kwa njia ya ukali. Anajileta kwa wema wa kibinadamu, kama malaika wa nuru katika nia na mawazo yako.
11/ Tuchunguze Maandiko mengine yanayotupatia taswira ya mapambano na vita yetu:
2 Wakorinto 10: 3, 4
“Kwa maana hata tunatembea katika mwili, hatufanyi vita kwa namna ya mwili; (Maana silaha za vita yetu si za mwili, lakini zina uwezo katika Mungu kuangusha maboma ya vita);”
Tunaambiwa mara tena ya kwamba sisi tunatembea katika mwili, bali vita vyetu si vya mwili hata kidogo.
Kwa sababu silaha za vita vyetu si vya mwili, lakini vina uwezo katika Mungu kuangusha maboma ya vita, inamaanisha kwamba vitani mwetu twapashwa kugandamiza adui, twapashwa kumuangushia silaha zetu nzito Sawa sawa na namna adui alivyofanya hapo kale.
Wakati walipopenda kuzingira mahali kwa kuishika, waliizunguuka pande zote, wakishika na kufunika milango yote na ni hapa sasa walipashwa kuangusha maboma. Je ni maboma gani?
Ni maboma gani yanayopashwa kuzingira?
Ni mawazo, mafikiri, na kuweka kila nia na mawazo kwa utumwa chini ya
kutii Kristo.
Kiisha kuyashinda na kuvunja mawazo na mafikiri, ni nini inayotegwa nyara na kushikwa?
Yanayoshikwa ni mawazo.
Tunapigwa vita na Shetani katika nia na mawazo yetu na mapambano hayo ni ya ana kwa ana.
12/ Wakolosai 3: 2
“Tieni mafikiri yenu juu ya maneno ya juu, wala si juu ya maneno yaliyo duniani.” Tumeambiwa hapa kwamba tuweke mafikiri yetu juu ya maneno yaliyo juu. Hatupashwi tu kutarajia kwenda mbinguni na kutafuta mbingu, bali mafikiri yetu yapashwa kuelekea mbingu.
Nikusema kwamba neno “kutamani” yamaanisha mafikiri ama mawazo Tunapashwa kuwa na mawazo yenye saa zote yafikiri tu mambo ya mbinguni siyo mambo ya duniani.
Twapashwa kufikiri Kristo, hii ndiyo vita vyetu.
Wakati tunafikiri Kristo, Shetani na majeshi zake mapepo wachafu wanahitaji tufikiri maneno mengine pahali pa kufikiri Kristo.
Maneno yale na vifaa vile kweli vyatufaa maishani mwetu, bali vifaa vile na maneno yale siyo ya Kristo, na ni hiyo vita tunavyo.
13/ Wafilipi 4: 8
“Kwa kumaliza, ndugu zangu, maneno yo yote yaliyo ya kweli, maneno yo yote yaliyo ya heshima, maneno yo yote yaliyo haki, maneno yoyote yaliyo safi, maneno yo yote yenye kupendeza, maneno yo yote yenye sifa njema; ukiwa wema wo wote na ikiwa sifa yo yote fikirieni maneno haya.”
Ningetamani muweke mukazo kwa maneno mawili hapa:
Katika aya ya nane tunaambiwa kuwaza haki sambamba yenye haki.
Na katika aya ya kenda twaambiwa kutenda haki.
Ni kusema kwamba ukiwa na mawazo sambamba yenye haki, kwa urahisi wote utatenda haki.
Hii ndiyo jambo la musingi, utaratibu wa kinidhamu katika mafikiri yetu. Kweli tutaambatana na kufanana na yale tunayofikiri.
14/ Waroma 12: 1 – 3
“Kwa sababu hii, ndugu, ninawasihi ninyi, kwa rehema za Mungu, mutoe miili yenu iwe zabihu iliyo hai, takatifu, ya kupendeza Mungu, ndio utumishi wenu ulio na maana. Na musifananishwa kwa namna ya dunia hii; lakini mugeuzwe kwa kufanya upya nia zenu, mupate kujua sana mapenzi ya Mungu, yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Kwa sababu kwa neema niliyopewa, ninamwambia kila mtu wa kwenu, asiwaze kujisifu kupita ilivyompasa kuwaza, lakini awaze kwa akili, kama Mungu alivyogawia kila mtu kadiri ya imani.”
Tambueni kwamba ni haya Shetani hatamani nyinyi kufanya.
Kumtia Mwenyezi Mungu mbele ya maneno yote, kujitowa wewe mwenyewe kwa Mungu kama sadaka iliyo hai.
Shetani hapendi jambo hili, kwa hiyo anahitaji nini?
Anahitaji kupotosha mafikiri yako isifikiri namna sawa, ndiyo maana Mwenyezi Mungu anatuomba tugeuzwe kwa kufanya upya nia zetu, na wakati nia yako inafanywa upya, wewe utakuwa na akili na utajiwaza na kujiona sawasawa na ginsi inavyokupasa kuona utu wako, hauta kuwa mwenye kiburi na kujisifu.
Wewe hautajiona kuwa juu ya wengine na kuwa mwenye nguvu na uwezo wote kupita wengine.
AMINA
N°Ref: 01/01/1961 / 28 - THE STRATEGY OF THE MOCK ANGEL / 09/22/2021
No comments:
Post a Comment