Saturday, April 30, 2022

UTAFANANA NAMNA GANI KWA NYAKATI ITAKAO KUJA / HOW WILL YOU LOOK IN THE FUTURE




UTAFANANA NAMNA GANI KWA NYAKATI ITAKAO KUJA 

HOW WILL YOU LOOK IN THE FUTURE 

March 14, 1965

Pastor Henry F. Kulp 





 

Waroma 8: 17 – 19 

“na kama sisi, basi tu wariti: wariti wa Mungu na wariti pamoja na Kristo; kama tukiteswa pamoja naye, ili tutukuzwe pamoja naye vilevile. 

Kwa maana ninahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu tukiyafananisha na utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. 

Kwa maana viumbe vyote vinangojea kwa hamu sana ufunuo wa wana wa Mungu.” 

         Hapa Mwenyezi Mungu anazungumuzia mwamini kama muriti pamoja na Kristo, sisi tutakuwa wariti pamoja na Kristo katika yote na ndani ya yote. 

Sisi si wariti tu, lakini sisi ni wariti pamoja na Kristo. 

Uriti wetu ndani ya Kristo hautagawanyika. 

Hauta gawanyika kamwe kwa sehemu mbalimbali na hii ni jambo maalum umbalimbali na kuwa mwanamemba wa ufalme wa hapa duniani kwenye urizi unagawanywa kwa sehemu.  


1/ Mwenyezi Mungu anasema tena kwamba:  

… kama tukiteswa pamoja naye, ili tutukuzwe pamoja naye vilevile. 

Kwa maana ninahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu tukiyafananisha na utukufu ule utakaofunuliwa kwetu.  

Kwa kweli kuna neno lisilo andikwa hapa, lakini lenye kufaa sana katika wazo hili, na  ni neno la muhimu sana katika maisha ya kikristo. 


2/ Mbele niwajulishe neno lile, nataka kwanza tufikiri kuhusu jambo moja. 

Kwa kweli, kuna wapagani kazaa wenye kutizama maisha ya wakristo na wanasema: 

Sina kitu cha kutamania zidi ya maisha ya wakristo, kwa sababu sioni jambo njema wanalo lenye mimi sina. 

Wao, wanakumbwa na shida na matatizo aina yote yenye inayonikumba, pia wao hupata ajali kama mimi. 

Ninafahamu wengi wa watoto wa Watumishi maalum wa Mungu, walioishi maisha ya kumucha Mungu na utawa, na watoto wao vilevile walisema maneno kama yale, sababu waliona kiwango gani wazazi wao walisumbuka, wakiwa na maisha ya tabu, kwa hiyo, sioni jambo la kutisha  na kuvutia katika maisha ya kikristo. 

Kwa hiyo, jameni muacheni mimi niende inje, nikijifurahishe, nile, ninywe na nipitishe saa katika anasa na raha. 


3/ Wengine wanaojitahidi kuwa marafiki wa Biblia, wakijiita wakristo  wanajitwika bidii ya  kupima kubadirisha hali hili. 

Wanasema kwamba kanisa ilishindwa kutumia zawadi zake za kiroho na yakuwa, kwa kupata baraka hizo, sharti wewe uwe yule mtu mwenye kuambatana na hali yenye Mwenyezi Mungu anataka wewe kuwa. 

Ukiheshimu mwenendo huo, wewe utakuwa na gari nzuri sana kwa mahali pako, utaishi katika gorofa nzuri, ndaa yako itajaa na pesa, utakuwa na kazi nzuri na afya ya mwili wako itakuwa nzuri. 

Lakini kwa wepesi, unapotizama watu wale, utatambua kwamba hakuna hata kitu moja kinacho timilika ndani ya maneno yote wanayoyasema. 

Hakuna kile kinacho timilika. 


4/ Neno hili fupi tunalopenda kuwafunulia, ni jambo ambalo twapasha kufahamu, ni neno “Subiri” 

Mungu hakutuahidi vifaa na hazina vya hapa chini duniani, lakini anatuahidi nyakati itakao kuja ya utukufu.   

Kwa mfano, hapa kwa kanisa letu la fasi, tunatarajia majengo ya shule ya jumapili ama nyumba yenye watoto watatumia kwa ibada yao ya watoto, pia tunatarajia kuwa na kitengo cha elimu na maadibisho, hapa kwa kanisa letu la Altoona Bible Church. 

Sisi tuko kwenye changamoto ya kuendelesha na kutimiza miradi na mkakato wa yale majengo. 

Tuna mbunifu mjenzi ama mjengaji mkuu anayefanya taswira ya majengo haya yote, na mipango haya yote yataoneshwa kwenu, na kweli mutayaona. 

Mistari hii iliyochorwa kwenye kartasi, siyo nyumba, baadaye itafaa kuweko mkataba na masikilizano kuhusu kazi, na kwa mwisho wajengaji wataanza kuchapa kazi. 

Wajengaji watapandisha ukuta ya sehemu zote wakifuata kwa makini sana picha iliyochapwa na mjengaji mkuu, sawa vile  alivyochora kwenye kartasi.

Nasi vilevile, Mjengaji wetu Mkuu ni Mwenyezi Mungu, Yeye anatupatia ahadi kuhusu nyakati zitakazokuja, anatuchorea mipango yake na miradi yake ndani ya Maandiko Matakatifu. 

Na siku moja wakati tutakapokwenda kukutana naye uso kwa uso, yote tuliyo tarajia tutayaona waziwazi kwa mecho yetu wenyewe. 

5/ Kila mara wakati ninaposoma maandiko ya Waroma 8, mafikiri yangu yanakwenda pale pale kwa Maandiko ya 2 Timoteo 4: 7 – 8, 

“Nimepiga vita vizuri, nimemaliza mwendo wangu, nimelinda imani; nyuma ya haya nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana mhukumu wa haki atanipa siku ile; wala si mimi tu, lakini watu wote pia wameopenda kuonekana kwake.” 

         Mtume Paulo amesema hapa kwamba amepiga vita vizuri, amemaliza mwendo wake, pia amelinda imani, kwa muda huu, kama mutakumbuka, Mtume Paulo alikuwa anangojea kuuwawa, tayari walijitayarisha kumukata kichwa na alikuwa tayari kukutana na Bwana Yesu Kristo. 

Tizama sasa neno la kwanza la aya ya nane. 

“Nyuma ya haya” neno la kuvutia na la muhimu. 

Wewe, maishani mwako, unayo neno la kufanana kama neno “nyuma ya haya”? 

Neno hili latuangazia kwamba nyakati itakao kuja itakuwa ya raha na heshima kubwa. 

Je, maishani mwako, neno unayo yafanana tu na “sasa hivi”, hapo hapo”,  ama unayo vilevile neno “nyuma ya haya”? 

Kwa kweli, mukristo  anaishi kwa kungojea  “nyuma ya pale nimewekewa”. 


6/ Tuchunguze sasa yanayosemwa kwa aya ya 18, (Waroma 8: 18) 

…utukufu ule utakaofunuliwa kwetu. 

Hapa tuna jambo maaulum sana kujifunza. 

Biblia inatuambia kuhusu utukufu yenye kuumbwa na utukufu usioumbwa. 

 

1 Wakorinto 15: 41 

“kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwengine wa mwezi, na utukufu mwengine wa nyota; kwa sababu nyota moja inautukufu mbalimbali na nyota nyingine.” 

         Hapa mtume Paulo anatuzungumuzia kuhusu Ulimwengu, anatueleza kwamba kuna utukufu ndani ya jua, kuna utukufu mwengine ndani ya mwezi, pia kuna utukufu mwengine ndani ya nyota. 

Na nyota moja inautukufu mbalimbali ya nyota nyingine. 

Haya yote yanakuwa na utukufu yenye siku moja itatoweka, siyo utukufu wa milele. 

2 Petro 3: 10 

“lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hii mbingu zitatoweka na sauti kubwa, na viumbe vya asili vitayeyushwa kwa moto mkali, na inchi na kazi zilizo ndani yake zitateketezwa.” 

         Hii siyo utukufu wenye tutakuwa nao. 


7/ Tukumbuke kwamba 1 Wakorinto 15: 43, inasema kwamba: 

“unapandwa katika haya; unafufuliwa katika utukufu: unapandwa katika uzaifu, unafufuliwa katika uwezo;” 

         Mwili wa ufufuko, ulipandwa katika kuoza, unafufuliwa katika kutokuharibika. 

unapandwa katika haya; unafufuliwa katika utukufu: unapandwa katika uzaifu, unafufuliwa katika uwezo. 

Tunaona hapa hali tatu mbalimbali sana yanayoonesha hali ya mwili.  

 

Kwanza wakati mwili unazikwa kwa udongo,   pia wakati wa ufufuko. 

Kwanza tunapandwa katika haya ya kuoza, tunafufuka katika hali ya kutokuharibika. 

Kuoza yaonekana wazi na mwili wa mufu unazikwa katika hali hii ya kuoza. 

Mwili unaoza. 

Na Watumishi wa Mungu wanasema: “Mavumbi wewe, utarudi kwa mavumbi.” 

Nazani ni vema turudishe mafikiri yetu katika Maandiko ya Yoane 11: 39  

Hapa Marata yuko mbele ya kaburi ya kaka yake na anasema:

“Yesu akasema: Mwondoshe jiwe. 

Marata, ndugu mke ya yule mtu aliyekufa, akamwambia: Bwana ananuka sasa; maana, amekuwa maiti siku ine.” 

         Hali ya kutokuharibika ni umbalimbali na kuoza. 

Kutokuharibika ni hali isiyo ya muda, ni ya milele, kamili, isiyo na kivuli ya kugeuka. 


8/ Pia anasema 

Unapandwa katika haya; unafufuliwa katika utukufu. 

Ni kweli kwamba tunafanya yote iwezekanayo kwa kuleta heshima kwa mwili wa marehemu wakati wa mazishi. 

Tunatafuta mavazi mazuri, sanduku nzuri, maua, tunajipanga kwa mustari mbele ya sanduku ya marehemu ili tumutazame kwa mwisho, kiisha tunaendelea na mazishi, na haya yote ni vema. 

Bali, kwa muda huohuo, mwili mwenyewe unaanza kuoza, hali ya haya, tunaanza kujiharakisha ili tuutowe kando yetu kwa woga wa kutokuvumilia matokeo ya mwili kuanza kuharibika na kuoza na hatutaki kufikia kiwango cha kutokuvumilia harufu mbaya ya mwili kuoza. 

Bali, mwili wenye tutakuwa nao kwa ufufuko, utakuwa mwili wa utukufu. 

Jameni, bila shaka, mwili huo utakuwa wa utukufu. 

Hii ni sehemu ya utukufu yenye itakuwa yetu.

Waroma 8, inatuambia kuhusu nyakati hiyo, miili yetu itakuwa ya utukufu. 

Na itafananishwa na nini?  

Tujikumbushe kwa muda muchache jambo la Bwana Yesu kugeuzwa sura juu ya mlima. 


Matayo 17: 1 – 2 

“Na nyuma ya siku sita Yesu akatwaa Petro, na Yakobo, na Yoane, ndugu yake pamoja naye, na kuwaleta juu ya mlima mrefu peke yao; 

Akageuzwa sura mbele yao; sura yake ikangaa kama jua, na mavazi yake yalikuwa meupe kama nuru.” 

         Inasemwa kwamba sura yake ikageuzwa na ikangaa kama jua, na mavazi yake yalikuwa meupe kama nuru.  

Miili yetu itakuwa sawa na ya Bwana Yesu, kama vile tusomavyo katika 

Wafilipi 3: 21 

“atakayebadilisha mwili wetu wa haya upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uwezo ule anaoweza kutiisha vitu vyote viwe chini yake.” 

         Kwa wewe uliyeokoka kweli utarajie jambo hili, kwa sababu utakuwa na mwili wa utukufu. 

Tafakari namna unavyotunza mwili wako kila siku. 

Lakini siku moja, mwili peke yake utakuwa mwili wenye utukufu. 

Mbele ya siku chache, nilisoma katika gazeti Altoona mirroir, kwa sehemu iitwayo Siku ya sita mangaribi, na ilikuwa kuhusu mchezaji moja mwanamuke aliyekuwa murembo sana, lakini uzee ulimushambulia na anapoteza kungaa kwa urembo wake. 

Lakini utukufu tutakayopata haitatoweka kamwe, itakuwa nasi siku zote kwa milele. 

Nashindwa namna ya kueleza aina ya utukufu huo, bali ni utukufu  tutakaokuwa nao.  

Ni wajibu wetu kuisubiri kweli. 


9/ Baadaye, mwili wa kufa wenye unazikwa katika haya, 

 Ushujaa wote unatoweka, hakuna hata nguvu kidogo ya kumruhusu kupumua hata donge moja la pumzi. 

Mwili inapoteza uwezo na nguvu ya kupiganisha mashambulio yote ya nje inayosababisha mwili kuoza. 

Mwili unalala hapo ukiwa bila uwezo wowote wa kujikinga na mashambulizi yote ya asili. 

Ni hiyo hiyo mwili itakayoonekana baadaye katika uwezo. 


10/ Baadaye, tupime kufahamu mambo machache kuhusu utukufu. 

Yoane 17: 5 

“Na sasa unitukuze, Baba, pamoja nawe mwenyewe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe mbele ya kuwa dunia.” 

         Bwana Yesu Kristo, katika maombi yake hapa kama Kuhani Mkuu, aliomba Baba Mungu amurudishie utukufu wake aliokuwa nao katika umilele uliopita, mbele Bwana Yesu ajifanye kuwa mtu, akiacha kando ule utukufu wake. 

Hii ni utukufu wenye hauwezi kuumbwa. 

Ni utukufu wa milele. 

Ni utukufu unaodumu milele daima, sawa vile Mungu ni wa milele daima. 

Utukufu huu ni wa milele daima, kwa hivyo aliomba Baba Mungu amurudishie ule utukufu wake, na kweli Utukufu wake ulirudishwa kwake. 


11/ Bali, wakati Bwana Yesu alipokuwa akitembea duniani, Yeye hakuonekana na huo utukufu. 


Marko 6: 1 – 3 

“Akatoka kule, akafika katika inchi yake mwenyewe; wanafunzi wake wakamfuata. 

Ilipokuwa sabato, akaanza kufundisha katika sunagogi. 

Watu wengi wakisikia, wakashangaa, wakasema: 

Huyu amepata maneno haya wapi? 

Na akili gani aliyopewa huyu? Na nini matendo ya uwezo yaliyofanyiwa na mikono yake? 

Huyu si seremala, mwana wa Maria, na ndugu ya Yakobo na Yose na Yuda na Simini? Ndugu zake wanawake si hapa pamoja nasi? Wakachukizwa naye.” 

         Wakati alipokuwa akitembea hapa chini duniani, Bwana Yesu alikuwa sawa sawa na mtu kawaida, sawa mtu wa aina ya watu kama desturi, na wao walimjuwa kama musermala. 

Kwa muda huo hakuwa hata na sehemu ya Utukufu wake, 

Alifanya maishara mengi na matendo ya ishara bila kuwa mtu wa hali ya utukufu, sawasawa nasi kwa siku za leo. 

Wakati tunapotembea na kujielekeza huko na kule katika mitaa yetu, hatuoni watu kushimama kwa kushangaa wakisema: Tazameni mtoto wa Mungu yule anayeelekea huko, ama tazameni mtu wa utukufu anayetembea. 

Hakuna mambo sawa na yale ijapokuwa mchana na usiku wanatutizama tukiwa kama mashaidi kwao. 


12/ Wakolosayi 3: 4 

“Wakati Kristo aliye uzima wetu atakapofunuliwa, nanyi vilevile mutafunuliwa pamoja naye katika utukufu.” 

         Sisi tutafunuliwa pamoja Naye katika Utukufu wake, na utukufu ule hautakuwa utukufu ulioumbwa, ni utukufu ambao, baada ya sisi kuupata, utabaki kwetu milele daima. 


13/ Tunavumbua kawaida ya mafundisho ya aina mbili katika Maandiko ya Wakolosayi 3: 4, sababu inasema kwamba wakati Kristo aliye uzima wetu atakapofunuliwa, nanyi vilevile mutafunuliwa pamoja naye katika utukufu.  

Neno kuonekana inatafsiriwa mu kigriki kwa neno kufunuliwa, pia vilevile kwa neno kumfunua. 

Nikusema kwamba kawaida ya mafundisho ya kufunuliwa na ya utukufu yanatimilika kwa nyakati moja. 

Wakati tutafunuliwa, tutatukuzwa.  

 

AMINA.


N°Ref: 03/14/1965 / 290 - HOW WILL YOU LOOK IN THE FUTURE / 04/30/2022

Friday, April 1, 2022

JAMBO LA KUTUSISIMUA KWA NYIMBO / SOMETHING TO SING ABOUT






JAMBO LA KUTUSISIMUA KWA NYIMBO 

SOMETHING TO SING ABOUT 

November 23, 1977

Pastor Henry F. Kulp




 

2 Timoteo 2: 11 – 13 


“Neno hili ni neno la kweli: Maana kama tukikufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye: 

Kama tukivumilia, tutamiliki pamoja naye: 

Kama tukimkana yeye, yeye atatukana sisi vilevile: 

Kama sisi hatuamini, yeye anakaa mwaminifu; maana hawezi kujikana mwenyewe.” 

         Tunayo hapa aya moja maaulum kweli toka Maandiko Matakatifu. 

Aya hizi tatu, zinahesabiwa kuwa sawa shairi ama pia wimbo wa taifa kwa Wasomi na maakili wenye ufahamu nyingi. 

Na yaonekana wazi kwamba, makanisa na makusanyiko ya hapo kale, tayari yalikuwa yakiyaimba.  

Nasi vilevile, kufwatana na namna tutaendelea na majifunzo yetu katika aya hizi, tutagunduwa kwamba kuna jambo maalum, njema na nzuri lenye laweza kutusisimua sisi kwa nyimbo.

 

1/ Hii ni neno muhimu sana na lenye manufaa kweli tunalopaswa kufahamu kwa mwanzo wa hutuba hili tunalo. 

Tuliwafahamisha kwamba kuna kanuni zinazo baki imara na kubaki daima katika kila Matunzaji, na hapo tunakuta jambo lenye kuonekana katika kila Utunzaji. 

Wao wanaofahamu Kawaida ya Mafundisho na kuyatumia katika mwenendo wao wa kila siku, wao watakuwa waamini wenye kuimba nyimbo. 


2/ Isaya 12: 2 

 

“Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu, nitatumaini, na sitaogopa: maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; naye amekuwa wokovu wangu.” 

         Nabii anatuambia hapa kwamba: 

Mungu ni wokovu wangu, nguvu yangu na wimbo wangu. 

Utatu wa namna gani! 

Ya kwanza, Mungu ni wokovu wangu. 

Hakungelikuwako uhusiano na Mungu kama mtu hangeliokolewa. 

Mwatambuwa vema kwamba Mungu ni wokovu. 

Sasa dini yajiwekea wokovu. 

Bali, bila wokovu, dini halingalifaa kwa kitu. 

Ya pili, Nabii anasema kwamba Mungu ndiye nguvu yake. 

Yamaanisha kwamba siku kwa siku twaishi kwa kumtwiga Bwana vyote. 

Ya tatu, anasema kwamba Mungu ni wimbo wake. 


3/ Waefeso 5: 18 - 19

 Hii ni jambo la ajabu sana lenye Mwenyezi Mungu analokabizi tu wale wenye kuamua kuhusiana na kutembea na Mungu. 

Hakuna yeye anayeweza kuhakikisha na kuzibitisha kwamba yafaa furaha iwe kwao wenye kuwa na wokovu. 

Mtu aweza kuwa mwamini bali bila kuwa na nyimbo. 

Kwa kweli, wengi kati ya wana wa Mungu wanaishi kati maisha inayo tembelewa na unyonge, kuna wanao kuwa na huzuni,  na hata manunguniko  katika hali namna sawa ni vigumu kuwa na  wimbo rohoni mwako; na kwa kweli  hii ni ungo la nyongezo. 


4/ Zaburi 40: 2, 3

 

“Akanipandisha vilevile toka shimo la uharibifu, toka udongo ulio mtelezi; 

Akaweka miguu yangu juu ya mwamba na kusimamisha hatua zangu.” 

Ameweka wimbo mupya kinywani mwangu, hata sifa kwa Mungu wetu, 

Watu wengi wataona na kuogopa, 

Na watawekea Bwana tumaini lao.”  

         Hapa tuna mzunguko wa tawasifu ya kiroho. 


(1) Akanipandisha vilevile toka shimo la uharibifu, toka udongo ulio mtelezi; hii ni neno la msingi. 


(2) Akasimamisha hatua zangu; hii ni jambo la kila siku, kila nyakati. 


(3) Ameweka wimbo mupya kinywani mwangu. 

Jambo nyingine la zaidi, siyo la muhimu kweli, lakini halali kuwa nalo. 


5/ Tena kwa mushangao mkubwa twasoma kwamba:  

Watu wengi wataona. 

Hapo hapo unasema kwamba: 

“Hii ni makosa, sababu, tafsiri lake lingepashwa kuwa, watu wengi watalisikia.” 

Siyo hilo, awali neno la asili linasema: watu wengi wataona. 

Siyo kosa, ni MATOKEO YANAYOONEKANA NA MECHO. 

Mtu anayeimba wimbo unaotoka humo ndani ya roho yake, anaionesha wazi kwa hali yake ya njee kwa kusisitiza na viungo vya maumbile yake. 

Kuonekana kwake kwa nje kunasema zaidi ya sauti analolitoa. 


6/ “Wala musilewe kwa mvinyo, ndani yake ni makelele, lakini mujaze Roho; 

Mukisemezana ninyi kwa ninyi kwa zaburi na tenzi na nyimbo za roho, mukiimba na kushangilia Bwana mioyoni mwenu;”  

         Katika waraka wa Mtume Paulo, tokeo la mwamini kujazwa na Roho Mtakatifu ni kuwa mwamini anayeimba. 

Jameni niwaonesha kwamba, hata Mtume Paulo naye vilevile alikuwa akiheshimu maagizo hayo. 

Yeye hatuambie neno ambalo lilikuwa kigeni kwake na lenye yeye mwenyewe hakutenda.  


7/ Matendo ya Mitume 16: 21 – 25 


“Tena wanafundisha desturi zisizo halali kwetu kupokea wala kuzifuata, kwa sababu sisi tuko waroma. 

Makutano yote wakaondoka, wakawakwendea kwa nguvu, watawala wakaondosha nguo zao, wakaamuru wapigwe kwa fimbo. 

Walipokwisha kuwapiga mapigo mengi, wakawatupa katika kifungo, wakaamuru mlinzi wa kifungo awalinde sana. 

Naye akipata amri hii akawatupa katika chumba cha ndani, akawafunga miguu kwa mikatale. 

Lakini katikati ya usiku Paulo na Sila walikuwa wakiomba kwa Mungu, na kumwimbia sifa, na wafungwa wengine walisikiliza.” 

         Hapo, Paulo ndani ya kifungo chenye uchafu na cha ndani, kiisha kuumia na mapigo ya fimbo na kuregea sana, amejazwa na Roho Mtakatifu na kuanza kuimba. 

Alipata kusudi la jambo la kumusisimua kwa nyimbo, hakujali magumu yaliyomukumba. 

Walimuweka ndani ya gereza ya ndani iliyokuwa chafu sana ikijaa harufu ya kuleta matapishi, bali mambo haya yote kazaa hayakumufazaisha na kupambazusha mafikili yake. 

Yeye alipokea jambo hilo la zaidi lenye kusemekana ndani ya Isaya na Zaburi. 

Ni jambo la muhimu kwetu kufikia lengo la kufahamu na kugundua ukweli unaokuwa ndani ya Maandiko ya 


2 Timoteo 2: 11 – 13 


“Neno hili ni neno la kweli: Maana kama tukikufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye: 

Kama tukivumilia, tutamiliki pamoja naye: 

Kama tukimkana yeye, yeye atatukana sisi vilevile: 

Kama sisi hatuamini, yeye anakaa mwaminifu; maana hawezi kujikana mwenyewe.” 

 8/ Tufikili sasa kuhusu wimbo huo na tugundue jambo moja la muhimu sana. 

Katika aya ya kumi, Mwenyezi Mungu anazungumuza kuhusu wokovu na utukufu wa milele, ama utukufu wa kudumu. 

Wokovu ni kwa waamini wote, bali wokovu yenye utukufu wa kudumu haipewi kwa kila mwamini. 

Hili ndilo neno la msingi tunalolipata katika tenzi tupatalo katika aya 11 hadi 13.  

 

9/ Kuna namna mbili mbalimbali ya kawaida ya mafundisho tunayoweza kuona katika tenzi hili. 

Katika aya ya 11: kwa maana kama tulikufa pamoja naye, jambo hili linahusu maisha.  

Ya pili kuna jambo kuhusu kumiliki. 

10/ Jambo la kuhusu kuishi pamoja na Kristo, haliambatani na uaminifu wa mutakatifu, lakini linaambatana na uaminifu wa Bwana Yesu Kristo Musalabani. 

Hii ndiyo Musingi wa Mafundisho ya Waroma. 

Sasa twapaswa kusoma namna hii: 

SISI TULIKUFA PAMOJA NAYE. 


11/ Waroma 6: 3, 4 


“Au hamufahamu, sisi sote tulio batizwa katika Yesu Kristo, tulibatizwa katika kufa kwake? 

Hivi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika kufa kwake: hata kama Kristo alivyofufuka toka wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo tutembee katika upya wa uzima vilevile,” 

         Tufahamu kwamba wote waliobatizwa katika Kristo, walibatizwa katika kufa kwake, na ubatizo huu hauwezi kamwe kulinganishwa na ubatizo wa maji, jambo hili haliwezi kamwe kuwa vile, sababu haiwezekani. 

Tupate mwangaza wa ufahamu kwa njia ya Maandiko ya Wagalatia 3: 27 

“Maana ninyi wote muliobatizwa na kuingizwa katika Kristo, mumevaa Kristo.” 

         Nikusema kwamba, kama wewe haujapata ubatizo huu, wewe hauja vaa Kristo. 

Inaonekana wazi wazi kwamba ni upumbafu mtupu kuzani kwamba maji yanaweza kufanya kazi hii. 


TUTAISHI PAMOJA NAYE VILE VILE. 

Yamaanisha kwamba kifo hicho siyo mwisho ya maneno bali ni mwanzo. 


13/ Aya ya 12. 

“Kama tukivumilia, tutamiliki pamoja naye,…” 

         Tunafikia sasa: 

Kama tukivumilia, tutamiliki pamoja naye: kama tukimkana yeye, yeye atatukana sisi vilevile.  

Jina la sarufi “Sisi” yaonesha kwamba ni waamini wanao tenda tendo. 

Hali hii ni kwa wakristo pekee, bali siyo kila mukristo ndiye anayeweza kuvumilia mateso. 

Wengine kwepesi wanamukana. 

Kumbukeni Maandiko ya 2 Timoteo 1: 8 – 12 – 16 

“Basi usione haya kwa ushuhuda wa Bwana wetu, wala kwa mimi mfungwa wake: lakini uvumilie taabu pamoja na Habari Njema kwa nguvu za Mungu; 

Ambaye alituokoa  akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, lakini kwa kadiri ya kusudi lake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa katika Kristo Yesu mbele ya nyakati za zamani na sasa imefunuliwa na kuonekana kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili kufa, na kufunua uzima na maisha yasiyokoma kwa njia ya Habari Njema. 

Kwa Habari Njema hii niliyowekwa mhubiri, na mtume, na mwalimu wa Mataifa. 

Na kwa sababu yake ninapata mateso haya vilevile; lakini sioni haya; maana ninamjua yeye ambaye nilimwamini, na ninajua kabisa ya kwamba anaweza kulinda ile niliyoweka kwake hata siku ile. 

Shika mfano wa maneno ya kweli uliosikia kwangu, katika imani na mapendo yaliyo katika Kristo Yesu. 

Ulinde kitu kile kizuri kilichowekwa kwako kwa Roho Mtakatifu anayekaa ndani yetu. 

Umejua habari hizi ya kuwa wote walio katika Azia wameniacha, katika hawa ni Figelo na Hermogene. 

Bwana awape rehema walio wa nyumba ya Onesiforo; kwa mara nyingi aliniburudisha, wala hakuona haya kwa sababu ya mnyororo wangu.” 

         Twapata hapa waamini wanaosikia haya ya kumushuhudia Bwana Yesu na haya ya Mtume wake Paulo.  

Wao hawapendi maisha yao yaambatane na Maandiko ya Mtume Paulo, sababu yanasamani fulani na namna wao wanatenda namna sawa, yeye vilevile atawakana. Si kwamba watapoteza wokovu. 


14/ Aya ya 13 

“Kama sisi hatuamini, yeye anakaa mwaminifu; maana hawezi kujikana mwenyewe.” 

         Aya hii inatuonesha kwa makini sana kwamba neno hili lamaanisha kwamba siyo jambo la kupoteza wokovu. 

Kama sisi hatuamini, yenye kujitafsiri kwamba, kama sisi hatustahili kuheshimu imani, yenye inamaanisha kwamba kama sisi hatusadiki, nikusema kwamba tunajizuiza kuonesha ni nini tunaloamini kuhusu ukweli wa neno lake, yeye anabaki mwaminifu. Yeye hata watupilia. 

Jambo ni kwamba yeye hatawapa zawabu, bali watapata uzima. Wao ni wenye kuokolewa. 


15/ Tuchunguze kwa makini maneno mane ya mwisho wa aya ya 13. 

Yeye hawezi kujikana mwenyewe. 

Utafsiri wa kigriki ungelikua: kwa kujikana mwenyewe, kwake haiwezekane, Yeye hawezi kamwe kufanya hivyo. 

Hiyo inamaanisha nini? 

Sisi ni kipande cha Mwili wake. 

Sisi tunaungana naye, sisi ni viungo vya Mwili wake, na kutuondowa kwa kututupa mbali inamaanisha kwamba anajikana mwenyewe, na jambo hili haliwezekane kwake. 

Hii ni moja ya aya kubwa katika Biblia inayozungumuza kuhusu Amani ya milele. 

Aya hizi tatu zinaelekea jambo la zawabu. 

Waweza kupoteza zawabu yako, lakini hauwezi kupoteza wokovu wako. 


16/ Turudi nyuma kidogo na tuchunguze yale yanayoelekea Ufalme wa Mungu, tufahamu maana yake. 

Juma iliyopita,tulitumia aya ya Luka 19: 17 – 19 

“Akasema: Vema, mtumwa mzuri; kwa sababu unakuwa mwaminifu kwa neno ndogo sana, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. 

Na wa pili alikuja, akisema: Bwana, feza yako imepata feza tano. 

Akamwambia: Nawe uwe juu ya miji mitano.” 

         Twapashwa kufahamu kweli kwamba hapo anazungumuzia kuhusu Ufalme wa Mungu, siyo kuhusu Kanisa Mwili wa Kristo. 

 Katika aya ya 11, katika mufano huo tunakuta vikundi vitatu. 

“Nao wakisikia maneno haya, aliendelea kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalema, nao walizania ya kama ufalme wa Mungu utaonekana mara moja.” 

         -Wanainchi walikuwa sawa wenyi kuwakilisha Taifa la Izraeli kwa nyakati ya muda fulani, kwa mwanzo wa huduma na hasa kwa mwanzo wa Matendo ya Mitume. 

 - Pia watumishi ni kweli wao walikuwa watumwa wa Mungu na hiyo yaonekana, wao ni watumishi wake na anawaagiza wafanye biashara hata wakati atakapo kuja. 

Luka 19: 13 

“Akaita watumwa wake kumi, akawapa feza kumi, akawaambia: Fanyeni biashara hata wakati nitakaporudi.” 

-Watumishi wale wawili wa kwanza walikuwa waaminifu na wao walipata zawabu. 

Lakini sasa kwa aya 22 – 24,  

“Akamwambia: kwa kinywa chako nitakuhukumu, wewe mtumwa mbaya. 

Ulijua mimi ni mtu mkali, nikiondoa ile nisiyoweka, nikivuna nisiyopanda; 

Kwa sababu gani hukuweka feza yangu kwa wale wanaolinda feza, ninaporudi, niipate pamoja na faida? 

Akawaambia wale waliosimama karibu: Ondosha feza kwake, mukampe yule wa feza kumi.” 

         Hapa tuna mtumishi mubaya, 

Kumbukeni kwamba mtu huyu ni mtumishi. 

Hapa hawazungumuzie wokovu, bali ni jambo la zawabu. 

Na Bwana akamuondosha hiyo feza na kuikabizi kwa yule mwenye tayari alikuwa na kumi nyingine. 

Kwa aya ya 26, hapo anaonesha kanuni: 

“Kwani ninawaambia ninyi: Kila mtu aliye na kitu, atapewa; lakini yeye asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitaondolewa kwake.” 

Kukosa zawabu. 


17/ Aya ya 27 

“Lakini adui zangu hawa, wale wasiotaka nitawale juu yao, muwalete hapa, mukawaue mbele yangu.” 

         Hapa tuna maadui wa Bwana, wale wasiotaka Bwana atawale juu yao, Bwana aliamuru wawalete pale na kuwauwa mbele yake. 

Hawa watu hawakuokolewa. 

Wale sio watumishi, bali ni maadui. 


18/ 1 Wakorinto 3: 10 – 14 

“Kwa kadiri ya neema ya Mungu, niliyopewa, sawasawa mjenga mkubwa mwenye akili, niliweka msingi; na mtu mwengine anajenga juu yake. 

Lakini kila mtu aangalie namna gani anavyojenga juu yake. 

Maana mtu hawezi kuweka msingi mwengine ila ule uliokwisha kuwekwa, yeye Yesu Kristo. 

Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huu zahabu au feza, au mawe ya bei kubwa, au miti au nyasi au majani; 

Kazi ya kila mtu itaonekana wazi: Kwa sababu siku ile itaionyesha, kwa sababu itafunuliwa na moto; na moto utajaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani.” 

         Tunasikia hapa kwamba kwa mtu kupata zawabu, yafaa mtu huyu kujenga juu ya Msingi Yesu Kristo, ni Msingi uliokwisha kuwekwa na Mtume Paulo. 

Kama wewe siyo mufuasi wa mafundisho ya Mtume Paulo, wewe hutapokea zawabu. 

Tufahamu sana yanayosemwa kwa aya ya 15.

“Kama kazi ya mtu ikichomwa, atapata hasara: lakini yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.” 


19/ 1 Wakorinto 9: 27 

“Lakini ninatesa mwili wangu, na kuutumikisha, isiwe, nikikwisha kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.” 

         Hapa anaonekana kama mtu aliepona ajali ya kufa, aliepona kuangamia majini kwa kuzama, hii haioneshi kwamba alipoteza wokovu wake, lakini, anakataliwa kwa kupewa zawabu, na tukiendelea mbali na usomi hata kufika kwa aya ya 24, 25, tutatambuwa wazi kwamba inazungumuzia kuhusu zawabu.   

“Hamujuwi ya kuwa wale wanaopiga mbio katika mashindano, wote wanapiga mbio, lakini mmoja anapokea zawadi? 

Pigeni mbio namna hii; ili mupate. 

Na kila mtu anayeshindana, ana kiasi katika maneno yote. 

Basi wanafanya hivi kusudi wapate taji ya kuharibika: lakini sisi tupate taji isiyoharibika.”  

 

20/ Kutawala pamoja na KRISTO 

Waefeso 2: 6 

“na alitufufua pamoja naye na kutukalisha pamoja naye katika pahali pa mbingu, katika Kristo Yesu.” 

         Hapa inahusu  uwezo wetu na kiti chetu cha utawala katika pahali pa mbingu. 


21/ Sawa sawa na Taifa la Izraeli itakao miliki na kutawala kwa dunia kwa niaba ya Yesu Kristo, na wao watakuwa wajumbe wa Bwana Yesu Kristo (Ufunuo na wale watu 144.000) 

Sisi tutatawala kule mbinguni na tutakuwa wajumbe kwa viumbe vya mbingu. 

Isaya 61: 5, 6 

“Na wageni watasimama na watakulisha makundi yenu, na watu wa kabila lingine watakuwa walimaji wenu, na wenye kuchunga mizabibu yenu. 

Lakini ninyi mutaitwa makuhani wa BWANA; watu watawaita ninyi watumishi wa Mungu wetu; mutakula utajiri wa mataifa, na mutajisifu katika utukufu wao.” 

         Bali sisi tutakuwa makuhani wa Bwana kwa viumbe vya mbinguni, wao hawataweza kufahamu Neema, hawataweza kuitafakali. 

Wanatutazama kwa nyakati hizi nao hawana uwezo wa kufahamu Neema, ni wajibu wetu kwa wakati ule kuwafahamisha Neema ni nini. 

1 Wakorinto 4: 9 

“Kwani ninazania ya kwamba Mungu ametutoa sisi mitume katika mwisho kama watu waliohukumiwa wauawe: kwa sababu tumekuwa matazamo kwa dunia, na kwa malaika, na kwa watu.” 

Waefeso 3: 10 

“ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulishwe na falme na mamlaka katika pahali pa mbingu;” 

 

AMINA 

 

N°Ref: 11/223/1975 / 261-2 SOMETHING TO SING ABOUT / 03/31/2022

Monday, January 31, 2022

SHETANI ANAJISUMBUA NA KAZI BURE / THE DEVIL’S HOPELESS JOB

Photo by B Smith from the kitchen door




SHETANI ANAJISUMBUA NA KAZI BURE 

THE DEVIL’S HOPELESS JOB

July 4, 1965 

Pastor Henry F. Kulp




 

Waroma 8: 28 - 34  

“Na tunajua maneno yote yanafanya kazi pamoja kuwapatia mema wale wanaopenda Mungu, kwa wale walioitwa kwa kusudi lake. 

Kwa sababu wale ambao aliwajua tangu zamani, aliwachagua tangu zamani wafananishwe na sura ya Mwana wake, ili awe Mzaliwa wa kwanza katikati ya ndugu wengi. 

Na wale ambao aliwachagua tangu zamani, akawaita vilevile; na wale ambao aliwaita, akawahesabia haki: na wale ambao aliwahesabia haki, akawatukuza vilevile. 

Basi tutasema nini juu ya maneno haya? 

Kama Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 

Yeye asiyeachilia Mwana wake, lakini alimtoa kwa ajili yetu yote, namna gani atakosa kutuletea vitu vyote pamoja naye? 

Ni nani atakayeshitaki wachaguliwa wa Mungu? Mungu ambaye anawahesabia haki; 

Ni nani anayehukumu? Ndiye Kristo aliyekufa, ndiyo, zaidi amefufuka, naye yuko kwa mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anayetuombea.” 

         Katika sehemu hii ya Maandiko tunafika kwa nafasi yenye Mtume Paulo anauliza: Basi tutasema nini juu ya maneno haya? 

Na hapo anatutolea maelekezo ya mambo saba. 

Kama Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 

Baadaye anasema: 

Yeye asiyeachilia Mwana wake, lakini alimtoa kwa ajili yetu yote, namna gani atakosa kutuletea vitu vyote pamoja naye?  

Neno tuliyopata kwa mwisho wa mafundisho yetu ya juma jana ilisemaka ifwatavyo: 

Yeye asiyeachilia Mwana wake, lakini alimtoa kwa ajili yetu yote. 

Mungu Baba alimtoa Yesu Kristo. 

Alimtoa kwa nguvu ya giza, nguvu ya Shetani, na hapo alimufanya kuwa zambi kwa ajili yetu. 

Mara tena yatupasa kufahamu kawaida ya mafundisho haya inayosema Mungu Baba kamtoa Mungu Mwana kwa ajili yetu sote.

Twende kusoma ndani ya Wagalatia 2: 20 inayosema hivi:

“Nimesulubiwa pamoja na Kristo, lakini ni hai; wala si mimi, lakini Kristo ni hai ndani yangu; na uzima nilio nao sasa katika mwili, ni uzima wa Imani iliyo ya Mwana wa Mungu ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” 

         Neno “kwa ajili ya” ingelipashwa kuwa pale na tungesoma: 

Aliyejitoa nafsi yake Yeye mwenyewe kwa ajili yangu. 

Hii misemwa ni sawasawa na yale tunayoyapata katika musingi wa maneno tunayo katika tafsiri ya neno “kutoa kwa ajili ya” tunayopata katika Waraka wa 

Waroma 8: 32: Mungu alimutoa kwa ajili ya. 

Aliingia kwa shamba la Gestemani, kwa shabaa ya mapenzi yake yote. 

Yeye alitamka mara tatu: Baba, Baba, Baba, mapenzi yako yafanyike. 

Kiisha akatoka na kujitowa mwenyewe kwa mikono ya watesi wake. 

Alifanya hivyo kwa ajili yetu. 

Hakuna hata mtu mmoja anayeweza kutafsiri, kama ipasavyo, mateso na uchungu wa kuzidi wenye Mwana wa Mungu alioupata katika mapito yale ya uchungu, na unyonge na mateso makali. 

Ilikuwa jambo la mushangao na kutisha sana wakati alipojitoa Mwenyewe kwa ajili yako na mimi. 


1/ Tusome ndani ya waraka wa Waebrania 9: 14   

“basi si zaidi Damu ya Kristo, ndiye kwa Roho ya milele, alijitoa mwenyewe kwa Mungu, kuwa zabihu isiyo na alama, itasafisha zamiri zenu na matendo ya kufa, mupate kutumikia Mungu aliye hai?” 

         Damu inatajwa mara kumi na miwili katika Waraka huu. 

Inatuambia kuhusu kazi na umuhimu wa Damu na mambo gani Damu ilitimiza. 

Bila kumwanga Damu, hakuna ondoleo ya zambi.  

Kwa siku za leo, watu wanajaribu kuweka kando Damu ya Kristo, lakini hakuna yeyote atakayeweza kusadiki mafundisho ya Biblia na kuhepuka Damu ya Kristo. 

Damu ndiyo musingi wa wokovu wetu, na yakupasa kweli kweli kuamini Damu ile. 


2/ Sitaweza kusita kutangaza imara kwamba Wokovu ndiyo kazi ya muhimu na ya maalum sana ya Mwenyezi Mungu. 

Kama tunavyo fahamu, hakuna hata kazi moja katika uumbaji iliyo kuwa nzito na kuwa bei kali mbele ya Mungu. 

Hata hapa sasa, Mwenyezi Mungu anaweza kuamuwa kuumba ulimwengu ungine mupya na hiyo siyo shida kwake. 

Bali kuna jambo moja iliyofanya Mungu kuwa maskini, ni wakati Mungu Baba alimtoa Mungu Mwana aliyejitoa mwenyewe.

 

3/ Tuchunguze sasa yanayosemwa katika sura hii, tuendeleapo usomi: 

 Ndiye kwa Roho ya milele, alijitoa mwenyewe kwa Mungu 

Hili neno tunalipata tena kwa waraka wa Waroma 8: 32, pia ndani ya Wagalatia 2: 20. 

Tungelipashwa kusoma namna hii: 

Ndiye kwa Roho ya milele, alijitoa mwenyewe bila kilema wala alama. 

Mutafsiri alisahau neno “kwa ajili ya” 

Fundisho tunalopata hapa ni kwamba, kwa kujitoa Yeye mwenyewe kama Sadaka, Bwana wetu Yesu alikuwa na haja ya musaada wa Roho Mtakatifu; na hapo hapo tunamuona vile vile Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu akitumika pamoja ili Yesu Kristo atolewe kwa ajili ya zambi zetu.

  

4/ Waroma 8: 32  

“Yeye asiyeachilia Mwana wake, lakini alimtoa kwa ajili yetu yote, namna gani atakosa kutuletea vitu vyote pamoja naye?” 

         Tuangalie kwa makini sehemu ya pili ya aya hii: 

Namna gani atakosa kutuletea vitu vyote pamoja naye?   

Wakati Mungu Baba alimtoa Mungu Mwana wake kwa ajili yetu, Yeye alitupatia yote aliyokuwa nayo wakati alimutoa Mwana wake kwa ajili yetu. 

Katika utafuti wangu kuhusu china ya neno, niligunduwa kwamba msemwa: “kuletea vitu vyote” inatafsiriwa na neno: kutoa bila shaka ama shurti, ama bila malipo ama kutarajia kitu fulani baadaye. 

Yatupasa kufahamu haya mbele ya mambo yeyote. 

Mwenyezi Mungu hauzishi kitu. 

Mwenyezi Mungu si mwenye kutarajia masikilizano ya bei ya kitu fulani na wanadamu ili wapokee kitu toka kwake. 

Mwenyezi Mungu ni mwenye kututolea akitukabizi vyote. 

Mwenyezi Mungu yuko na zawadi kwa ulimwengu. 

Tafsiri maalum yenye ninaweza kuwa nayo kwa msemwa “kuletea vitu vyote” ni “kutoa kwa kukabizi yote bila mashito yoyote”. 

Tukirudi nyuma kidogo katika historia ya Inchi yetu, wakati Serkali iligawanyia watu viwanja kwa bure, shurti moja lenye kila aliyepata udongo alilopashwa kufanya, ni kwenda tu kwa udongo aliyopewa kushurulika nalo na kulimiliki na kulifanya kuwa mali yako binafsi.  

Ni hiyo tu ilimupasa kufanya, hakukulazimishwa hata malipo fulani, hakukukuwa hata mabishano, hakukukuwa kamba yenye iliyokuwa ikifungwa kwa zawadi ile, jambo lilikuwa tu la toleo ya zawadi ya sehemu ya ardhi bila malipo toka kwa Serkali.  

Hii ndiyo aina ya misemwa inayotumiwa hapa: 

Kuletea vitu vyote. 

Mwenyezi Mungu alitutolea bila malipo zawadi kubwa na yote aliyokuwa nayo wakati alipotutolea Mwana wake. 

Kwa sababu hiyo imeandikwa: 

Mambo yote ni yetu.

Nikifahamu kwamba Mwokozi Yesu Kristo ni wangu, mimi ninahaki ya kusema hivyo, ninaweza kusema kwa urahisi wote kwamba: Muumba wa ulimwengu wote, Yeye ni wangu. 

Yeye ni mali yangu, na vilevile wapashwa kufahamu kwamba wewe vilevile ni mali yake.  

Wakati Mwenyezi Mungu alitutolea Bwana Yesu Kristo, hapo alitupatia zawadi bila malipo ya ulimwengu wote kwa wale wenye kumuamini Bwana Yesu Kristo. 

Jambo hili ni la muhimu sana, unapashwa kumuamini Yesu Kristo. 


5/ Kuna hadisi lenye napenda kuwahadisia: 

Tayari mumekwisha kulisikia hapo mbele, lakini nazani kwamba haitakuwa mauzi kwenu kama ninawaadisia mara tena.   

Ni hadisi ya mtu moja aliyekuwa na mali mingi sana. 

Mke wake alifariki na akamuachia mtoto kijana mwanamume. 

Mtoto yule ndiye alikuwa yote kwa mtu yule. 

Na yeye aliweka kijakazi mwenye atakuwa akihusika na kulea mtoto huyo na kushurulika na haja zote za yule mtoto, na kijana huyu aligeuka kuwa sawa mtoto wa huu kijakazi, na kwa kweli ni hivyo tu njo ingepashwa kutukia. 

Huyu mtoto kijana mwanamume alikomaa na akafikisha umri wa miaka makumi mawili kiisha kwa gafla, akafariki. 

Mtu yule mutajiri akavunjika moyo sana, roho yake ikaumizwa sana kupita kiasi. 

Akajikuta kwamba dunia haifai kitu tena kwake na kwa kweli yeye hakugawa tena na kutoweka. 

Hakuna mtu aliyefahamu maelekezo gani iliyopangwa kuhusu hazina ya mtu huyu. 

Walitafuta huku na kule wakiangalia kila kartasi waliokuta, lakini hawakupata agano la mapenzi ya mwisho ya aliyefariki, hata kufika kiwango cha Serkali kushurulika na mambo haya, na kuchukuwa mali yote sababu hakukukuweko murizi, ama habari kuusu maandiko ya mapenzi ya mwisho ya marehemu. 

Ushuru ulifaanyika, vifaa vyote vya nyumbani hata na vitu vyote vya samani, vyote viliwekwa kwa bei ili kuuzishwa. 

Huyu kijakazi mama mlezi wa huyo kijana, naye alifika hapo, na kushimama wima kwa pembe moja la ukuta, naye hakuwa na pesa ila tu kiwango ndogo sana, yeye hangaliweza kujiuzia vitu vile vya samani, kwa hivyo, kwa ukuta, kulikuwa kungali picha ya kijana huyo na mecho ya kijakazi huyo ilikuwa tu ikielekea kwa picha ile aliyotamani na kuhitaji kwa moyo wake wote. 

Picha hiyo ilimufanana kweli kijana huyo marehemu aliyemupenda kwa moyo wake wote. 

Na ikafika wakati ya kuuzisha picha hiyo, hakuna hata mwenye alishurulika nayo. 

Mama mlezi huyo akanunua picha hiyo kwa bei ya chini mno, senti kama ngapi. 

Na alibeba picha hiyo nyumbani kwake. 

Akaipanguza na angalisho yote kwa saa za kutosha na baadaye akaiweka kwenye ukuta na hapo ikafanya miaka mengi. 

Na siku moja wakati alipokusudia kufungua kada ya nyuma, gafula, vikartasi kazaa vikaanguka chini, na kweli kwa mecho yake, vikartasi vile vilionesha sura ya kuwa vyenye mafaa na umuhimu sana. 

Baadaye, akakusudia kubeba vikartasi hivyo kwa Mwanasheria. 

Huyo Mwanasheria akamwambia, mwanamke, kwa sasa mana imekuangukia toka mbinguni na imeanguka kwa miguu yako, sababu huyo bwana marehemu mutajiri aliacha urizi wa mali yake yote kwa mtu ambaye alimpenda sana mtoto wake, hata kufika kiwango cha kununua hii picha iliyomfanana sana mtoto wake mwanaume. 

Yeye aliachia huyo mtu azina na mali yake yote. 

Mwenyezi Mungu anakutolea VYOTE kama wewe ukimupenda Mwana wake. 

Anakupatia vyote bila malipo yeyote, kama ZAWADI BILA MALIPO.


6/ Waroma 8: 33 – 34 

“Ni nani atakayeshitaki wachaguliwa wa Mungu? Mungu ambaye anawahesabia haki; 

Ni nani anayehukumu? Ndiye Kristo aliyekufa, ndiyo, zaidi amefufuka, naye yuko kwa mkono wa kuume wa Mungu, tena ndiye anayetuombea.” 

     Jambo muhimu la kutiya mkazo ni, kukumbuka neno lililokuwa kwa mwanzo wa Waraka huu wa Waroma sura ya nane, mara tena ni neno lilelile linalotumikishwa hapa. 

Kwa aya ya kwanza tunasoma:  

“Sasa, basi hakuna hukumu ya azabu juu yao walio katika Yesu Kristo, wasiotembea kufuata maneno ya mwili, lakini kufuata maneno ya Roho.” 

Na hapa kwa aya ya 33, tunapata hakikisho ya neno lile kwa sababu anatuambia kwamba, usipo amini, wewe wajiweka mwenyewe kwa nafasi ya hukumu. 

Nina swali la kuwauliza: 

Ni nani atakaye hukumu sisi? 

Ama ni nani kweli anayeweza kutuhukumu? 

Kama ni Mungu anayetuhesabia haki, ni nani basi anayeweza kujitia kwa nafasi ya kutuhukumu? 

Mungu ni muhukumu wa wote, 

Mungu ndiye Mahakama kuu. 

Wakati Mahakama kuu inaleta hukumu ya jambo lako, jambo lile limekomeshwa. 

Tayari Mahakama kuu imekwisha kutatua jambo lako, na Mahakama kuu ni Mungu na ni Yeye aliyesema: 

Ni Mungu ndiye anayehesabia haki. 

Kwa kumaanisha kwamba, anakukomboa toka migogoro yote, kukuweka huru toka migogoro yote, na kama Muhukumu anakuweka huru, ni nani yule atakayekuhukumu tena? Ni nani atakaye hukumu sisi? 


7/ Tuchunguze kwanza aya hii ya ajabu: 

Matendo 13: 39   

“na kwa yeye kila mtu anayeamini amekwisha kuhesabiwa haki katika maneno yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.” 

         Na kwa Yeye, Yeye ni KRISTO, kwa yeye kila anayeamini. 

Hii haimaanishi wale watu wanaozania kujiweka wenyewe kuwa wenye utawa kwa matendo yao wenyewe. 

Haimaanishi kuwa mushirika wa kanisa fulani, bali kuamini, kila mtu anayeamini. 

Ni pale twapashwa kuweka msingi wetu, hakuna jambo la kukadirisha. 

Kama ukileta swali kwa watu kumi, ukiwauliza kama tiyari wao ni wakristo, kenda juu ya kumi watakujibu kwamba: “Wako wanajikaza kutenda mema kwa kadiri wanavyoweza.” 

Mwenyezi Mungu haokowe kwa njia ile. Bali, kila mtu anayeamini anahesabiwa haki. Kwa mambo ngapi? Mambo yote. 

Kama wewe unahesabiwa haki kwa mambo yote, sasa ni nani atakayepata jambo la kuleta hukumu juu yako?

 

8/ Turudi nyuma kidogo kwa Waraka moja yenye watu wengi wanapendelea kutumia. 

Ufunuo 12: 10 

“Nikasikia sauti kubwa katika mbingu ikisema: Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye ambaye anawashitaki mbele ya Mungu wetu, mchana na usiku.” 

         Hii ni kwa nyakati ya Mateso Makuu, Shetani anakuwa akishitaki, wale wenye kuhubiri habari njema, wale 144000. 

Na hapo, kwa mwisho wa nyakati ya Mateso Makuu, Shetani mshitaki atatupwa chini toka eneo iliyokuwa yake. 

Kwa kweli, naamini kwamba hata kwa siku za leo kazi yake ni ile ile na anatumika namna sawa. 

Kumbukeni yale aliyofanya kwa Yobu. 

Yobu 1: 8 - 11  

“Bwana akamwambia Shetani: Umeangalia mtumishi wangu Yobu?

Maana hakuna mmoja kama yeye duniani, mtu mkamilifu na wa haki, mwenye kuogopa Mungu na kuepuka na uovu. 

Shetani akajibu BWANA akisema: Yobu anaogopa Mungu bure? Wewe hukumzunguka yeye na nyumba yake, na vyote aliyo navyo, kwa boma pande zote? 

Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake imeongezeka inchini. 

Lakini nyosha sasa mkono wako, na gusa vyote alivyo navyo, na yeye atakukufuru mbele ya uso wako.”  

         Hapa Shetani anaamua kumshitaki Yobu kwa Mungu. 

Ni baada ya Mungu kumtaja Yobu ndiyo Shetani baadaye alipata uwezo wa kumtaja. 

Shetani hangejaribu hata kidogo, bali ni Mwenyezi Mungu aliye muuliza eti umemwona Yobu? 

Ni kweli, wewe umemuzunguusha na boma la ukingo hata mimi siwezi kumutatiza, siwezi kumgusa Yobu. 

Na Shetani akaongeza akisema kwamba; uniruhusu nimunyanganye vitu vyote alivyonavyo, yeye atakukufuru mbele ya uso wako. 

Aya ya 12 

“Bwana akamwambia Shetani: Tazama, vyote alivyo navyo ni mkononi mwako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake mwenyewe, Basi Shetani akatoka mbele ya uso wa Bwana.” 

         Shetani alitwaa mali yote yenye Yobu alikuwa nayo katika dunia hii. 

Yobu alisema kwa aya ya 21: 

“akasema: Mtupu nilitoka tumboni mwa mama yangu, na mtupu nitarudi tena kule; Bwana ametoa, na Bwana ametwaa; abarikiwejina la BWANA.” 

         Mwatambua namna gani Shetani anapata haya, imeonekana wazi kwamba yeye ni mudanganyi. 

Shetani alikuwa akisema: Yobu atakukufuru mbele ya uso wako, bali Yobu hakutenda hivyo. 

Fundisho, tunalolipata katika Kitabu cha Yobu, kuhusu Shetani,  ni kwamba Shetani ni musema uongo, na wakati anapo washitaki watu, yeye anatumia uwongo.

  

9/ Mara tena Mungu alimuuliza kama alimwona Yobu, naye alijibu ndiyo 

Yobu 2: 4 – 6 

“Shetani akajibu Bwana, akasema: Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote mtu aliyo nayo atatoa kwa ajili ya uzima wake. 

Lakini nyosha sasa mkono wako, na gusa mifupa yake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako. 

Bwana akamwambia Shetani: Tazama, yeye ni mkononi mwako; acha uzima wake tu.” 

         Bali wewe uguse mwili wa Yobu naye atakukufuru, ngozi kwa ngozi, Shetani akasema uniruhusu niguse mwili wake, Mwenyezi Mungu akamwambia gusa mwili wake lakini usiguse uzima wake. 

Mungu akamwachilia Shetani kucheza na mwili wa Yobu hadi kiwango cha kwenda kukuna vidonda vyake katika majifu, mwili wote ukijaa majipu, vidonda na makovu. 

Naamini kwamba Shetani aliona kwamba hiyo njo machungu ya aina ya juu sana kuliko katika dunia hii. 

Alimuweka Yobu kuwa katika uharibifu wa kupita kiasi, uvunjaji wa hali ya ajabu, mwili kuharibiwa mno. 

Hata kama mambo haya yote yalitukia Yobu hakukufuru Mungu, hata hakumubebesha Mungu hukumu yeyote. 

Mara tena Shetani anaonekana kuwa mwenye uongo mno, yeye ni mwongo mkubwa sana. Wakati anaposhitaki watoto wa Mungu kuhusu mambo fulani, yeye anatumia uwongo mtupu. Yeye ni mwongo.

 

10/ Ni nini inayotukia wakati Shetani anatushitaki mbele ya Mungu Baba? 

   Ni nini inatukia wakati Shetani anageuza macho yake na kumuambia Mwenyezi Mungu eti tizama kwanza huko chini duniani na uone mambo wanayoyafanya wakristo.  

Kufa kwa Bwana Yesu ni kwa manufaa na muhimu sana kwetu, na pia tena Bwana wetu Yesu Kristo anatuombea akiketi kwa Mkono wa kuume wa Mungu Baba. 

Ni nini inayotukia wakati Shetani anafika mbele ya Mungu Baba na kumwambia tizama mtu yule Mary Smith ama John Tomes pale chini duniani, 

Wao ni wakristo, wao walimwamini Bwana Yesu Kristo, lakini tizama maovu wanayoyafanya. 

Tizama machafuko na machukizo na maovu wanayoyatenda, bali Bwana Yesu Kristo anasema: 

Ninayajuwa hayo yote, wao ni mali yangu na niko hapa kwa ajili ya kuwaombea. Mimi nilikufa kwa ajili yao. 

Nililipa malipo ya zambi zile, na zambi zile ziliwekwa juu yangu. 

Shetani anajaribu kukusanya mambo mengine mapya na kuyaleta mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini Mungu anamwambia, yote imekwisha lipwa, na kunakuwa harabuni ya hayo yote. 

Eti wafahamu kwamba ni vigumu na haiwezekani Shetani awe na ushahidi ya kwamba wewe unastahili hukumu? 

O kweli ninafahamu kwamba Shetani anajisumbua na kazi bure, kazi ya punda, kazi yenye haitamufikisha kwa lengo fulani. 

Anafahamu kwamba Biblia inasema kwamba zambi zetu zilitupwa mbali sana. 

Kwamba Mwenyezi Mungu alitukomboa na uzalimu wowote. 

Wewe binafsi waweza kujihukumu na kusema kweli Shetani anaweza akanishitaki kwa jambo hili na lile, hapana sivyo, Shetani hawezi kuleta ushahidi hata moja kwa sababu Bwana Yesu Kristo alibeba muzigo wako wote wa zambi na kuvaa hukumu iliyokuwa yako. 

Eti si Bwana Yesu alifanywa kuwa zambi? 

Kwa kweli, ni vigumu kwangu kusema zaidi ya hayo.

1 Yoane 4:17 

“Hivi mapendo yamekamilishwa kwetu, ili tuwe na uhodari katika siku ya hukumu; kwa sababu kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu.” 

Kwa kweli, Wakolosai 2: 10 inasema: 

“Na ninyi mumetimilika katika yeye aliye Kichwa cha falme zote na mamlaka.” 


11/ Katika Kigriki: 

NI NANI ATAKAYEJARIBU KUTUHUKUMU? 

MUHUKUMU MKUU YEYE MWENYEWE ALITUHESABIA HAKI BILA ZAMBI. 

Kama kuna yeyote yule anayependa kukushota zambi zako kidole, yafaa kwake kushota kidole chake kwake YEYE, na ni nani atakayejaribu kumshota?  

1 Petro 2: 24  

“Yeye mwenyewe alichukua zambi zetu katika mwili wake juu ya mti, hata sisi, tukiwa wafu kwa maneno ya zambi, tuwe hai kwa maneno ya haki, na kwa kupigwa kwake muliponyeshwa.” 

         Nani atakayejaribu kumshitaki? 

Ni Yeye anayeshitaki. 

Ni Yeye aliyechukuwa zambi zetu. 

Aliteswa kwa ajili ya zambi zetu.

 

12/ Waebrania 10: 11, 12 

“Na kila kuhani anasimama kila siku akitumikia, na kutoa zabihu zile zile mara nyingi, nazo haziwezi kabisa kuondoa zambi. 

Lakini yeye wakati alipokwisha kutoa zabihu moja kwa zambi hata milele, akiketi mkono wa kuume wa Mungu;” 

         Waraka wa Waebrania unalinganisha huduma ya Bwana Yesu Kristo na ya wale Makuhani wa Agano la Kale. 

Na kila kuhani anasimama kila siku akitumikia, na kutoa zabihu zile zile mara nyingi, nazo haziwezi kabisa kuondoa zambi. 

Lakini yeye wakati alipokwisha kutoa zabihu moja kwa zambi hata milele, akiketi mkono wa kuume wa Mungu; 

Tufahamu kwamba wakati Bwana Yesu Kristo alirudi mbinguni, Yeye aliketi sababu alitimiza na kumaliza kazi yake. 

Najua siku moja umekwisha kutenda kazi ya nguvu sana na baadaye unarudi nyumbani ukiwa tu na uwezo wa kuketi na kupumzika. 

Ilikuwa muhimu Bwana Yesu Kristu afanywe zambi kwa ajili yetu. 

Yeye alisulubishwa, na kufufuka toka wafu na kiisha alipaa kwenda mbinguni. 

Alirudi KWAKE. 

Anaketi kwa sababu kazi yote imekwisha. 

 Kwa hiyo, kumshitaki mwamini yeyote kwa jambo fulani alilolifanya, ingelimaanisha kusema kwamba kazi hii ya Bwana Yesu Kristo haikutimilika. Kwamba kazi hii haitoshi. 

Bali kwa uhakika na kweli kazi yake yote ilitimizwa, ni kwa hiyo, kama unahitaji kushitaki yeyote ule, unyooshe kidole chako na kushota Mwokozi wetu Kristo Yesu. Umshitaki tu Yeye. 

Usijaribu kushitaki hata moja ya watoto wake. 

13/ Tukumbuke pia kwamba Yeye anatuombea, akiketi, na kutuombea. 

Yeye hajajali kamwe kuwa na hali ya kasirani, Yeye hana haja ya kuwa na haraka haraka kama kuna mashitaki juu yetu, kwa sababu alitimiza kazi yote, yote imekwisha na anaendelea tu kusema: 

Mimi nilikufa kwa ajili ya mtu huyu. 

Nilikufa na kulipa malipo ya zambi zake. 

Sisi tumewekwa huru, sisi ni huru. 

 

AMINA.  

 

 N°Ref: 07/04/1965 / 30 - THE DEVIL’S HOPELESS JOB / 01/29/2022