Photo by B Smith from the Garden |
263 - NEEMA YA KAWAIDACOMMON GRACE
November 24, 1963
Pastor Henry F. Kulp
Waroma 2: 1 – 6
“Kwa sababu hii, huna uzuru, wewe mtu, mtu gani unayehukumu; kwa maana katika neno hili, unahukumu mwengine, unajihukumu mwenyewe; maana wewe unayehukumu unafanya mambo yale sawasawa.
Lakini tunajua hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wanaofanya mambo kama haya.
Na wewe mtu unazania unayehukumu wale wenye kufanya maneno yale, na unayafanya mwenyewe, ya kama wewe utakimbia hukumu ya Mungu?
Au unazarau utajiri wa wema wake na saburi na uvumilivu wake, usijue ya kama wema wa Mungu unakupeleka kwa toba?
Lakini kwa ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, unajiwekea akiba hasira kwa siku ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,
Atakayelipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;”
Ningelitamani tuhakikishe kwamba Maandiko ya Waroma 1: 20 inasema kwamba:
“Kwa sababu maneno yake yasiyoonekana, tangu kuumbwa kwa ulimwengu yanaonekana wazi, yanafahamika kwa kazi zake, hata uwezo wake wa milele na Uungu wake: Wasiwe na uzuru”
Kwa kweli kuna wale wasioweza kupewa radhi, wasioweza kuwa na uzuru, wasioweza kupata masamaa.
Mwenyezi Mungu anasema kwamba mtu hana uzuru, hawezi kusameheka, kwa maana mtu anatazama ushahidi unaoonekana wazi wa Muumba aliye Mungu asiyeonekana.
Ni kwa hiyo, wakati mtu husema kwamba: “Mungu hayuko, ama hakuna Mungu”, mtu huyu kweli anachanganyikiwa kama mwenye wazimu, na Mwenyezi Mungu asema kwamba mtu huyu hana uzuru.
Ni ya muhimu kwenu kufahamu yanayo zungumuziwa katika sura ya pili mustari wake wa kwanza, pahali Mungu anaposema kwamba:
“Kwa sababu hii, huna uzuru, wewe mtu”.
Hapo Mwenyezi Mungu anasema kuhusu mtu mbalimbali na yule tuliyeona kwa sura ya kwanza.
Kwa kweli, kwa sura ya kwanza, Mwenyezi Mungu alitufunulia kwamba wote wamefanya zambi na wote wanakuwa chini ya hukumu ya zambi nzito, bali anatuambia katika maandiko ya Waroma 1: 32 kwamba:
“hata walijua hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wanaofanya maneno kama haya wanastahili kufa, hawafanyi tu maneno haya, lakini wanakubaliana nao ambao wanayatenda.”
Mwenyezi Mungu husema kuhusu wale wanaoshangilia zambi zinazotendwa na wengine. Wakisukuma mbele zambi zinazokuwa katika wengine.
Tunayo mtu mwenye zambi, anayehakikisha kwamba ni uovu na kukubali kwamba ni hivyo, na anashangilia zambi anazoziona ndani ya wengine.
Bali kwa sura ya pili, tunayo picha ya mtu mwenye zambi, mwenye kuhukumiwa na zambi hizo, lakini anahukumu wengine.
Aya hii ya kwanza inatufunulia kwamba hatuna budi kuhukumu wengine.
1/ Jambo la msingi na la manufaa katika aya hii ya kwanza ni neno “kutokuwa na uzuru”.
Katika sura ya kwanza Mungu anauliza:
“Eti ninyi hamutazame ulimwengu na vyote vilivyoumbwa?”
Kama mwatazama, basi ninyi hamuna uzuru, sababu uumbaji na viumbe vyote vinavyoonekana vyanaonesha Mungu asiyeonekana.
Katika aya hii ya maandiko tunayosoma sasa anauliza:
Yawezekana umekwisha kuhukumu mtu ama kitu chochote?
Kwa hiyo, hauna uzuru, sababu hukumu yatoka kwenye zamiri, na zamiri tayari yatambua zambi iliyo ndani ya wengine sababu yajihukumu kwamba kuna hiyo hiyo zambi ndani mwake binafsi.
Katika siku zilizo pita tulisema ya kwamba zamiri ni matokeo la anguko la mwanadamu, na kwamba zambi unayotambua ni zambi yenye wewe mwenyewe tayari umekwisha kufanya kwa siku zilizo pita, na hapo hitimisho ni kwamba, yeyote mwenye atahukumu kitu chochote ndani ya mwengine, tayari kwa tendo lile anaandika hukumu yake mwenyewe.
2/ Hakuna yule asemaye kwamba mwenziwe husema uongo, bila lengo la kutaka kuficha mwelekeo wa kufunika ukweli.
Zamiri yako yakuhukumu kwamba wewe pia unafanya mambo yale yale, na mambo yale ni mbaya, na wakati unagundua mambo yale ndani ya wengine, hata nawe vilevile yanakuhukumu.
Sasa kwa kutaka kujisafisha na kuyahepuka, unajiweka kuhukumu wengine, kwa nia ya kuondowa zambi hiyo ndani yako.
3/ Hukumu, kukosoa, ama lawama lenye Mwenyezi Mungu anaturuhusu hapa katika Ulimwengu, ni hukumu, kukosoa ama lawama la wenye kutumia Neno la Mungu kwa kuonesha wengine kwamba wangali katika hali ya wenye zambi, kwamba dunia nzima imejaa zambi, siyo kwamba anayekosoa ni mwenye haki, lakini sababu anafahamu ya kwamba katika Biblia imeandikwa kwamba wote wamefanya zambi, na kwamba kuna Jibu ndani ya Bwana Yesu Kristo, anayehesabia haki wote wanaomwamini.
4/ Waroma 3: 2, 3
“Kuna faida sana kwa kila njia; kwanza kwa sababu walipewa maneno ya Mungu.
Ni nini basi, kama wengine hawakuamini? Kutokuamini kwao kutafanyiza uaminifu wa Mungu kuwa bure?”
Aya ya kwanza inatukataza kuhukumu ama kukosoa mwengine.
Kichwa cha aya ya 2: 3 yaweza kuwa: “hakuna uzuru”.
Sababu la muhimu lenye linatulazimisha tuwe tayari kwa kukutana na Mwenyezi Mungu, ni kwamba, yatupasa kukutana na Mwenyezi Mungu.
Katika jibu mbalimbali ya mahitaji na shuguli nyingi zinazotukumba maishani mwetu, kwa kawaida ya hapa chini duniani, kila mara kuna utaratibu ama kanuni tunayofuata sisi sote.
Waweza kumuuliza mtu fulani, sababu gani anajielekeza kwa mganga wa meno, eti kwenda kwa mganga wa meno ni jambo la kufurahisha?
Ni kweli kwamba hutajisikia mwenye raha wakati unakwenda kukutana na mganga wa meno?
Huyo mtu atakujibu: Kwa kweli jambo hili halinifurahishe kamwe, lakini, mimi ninajielekeza kwa mganga wa meno sababu ni lazima niende, sababu ni kwa mafaa yangu.
Mfano mwengine:
Mtu fulani anapoteza mpendwa wake na kiisha unamuuliza ndugu yake anayejielekeza kwa shamba la wafu kwa mazishi:
“Sababu gani unajielekeza kwa shamba ya wafu kuzika mwili wa mtu uliyekuwa unampenda sana? Je wataka mwili huu ugusane na vitu vyenye vitaharikisha mtengano wa viungo na kuboresha kuoza haraka? Eti, wewe hukuwa unampenda marehemu?”
Atakujibu:
Kwa kweli, ndiyo, nilimpenda, kwa nia yangu binafsi singelifanya hivyo, bali yanipasa kuzika huu mwili wa mpendwa wangu, yafaa kuuweka mbali nasi.
Mfano mwengine:
Unamzungumuzia mtu mwenye kukumbwa na kuzama sana ndani ya kazi akirejea mara kwa mara kwa hatuwa fulani ya kazi.
Unamuuliza, zababu gani unatumia chakula ama kinywaji kwa shida kabisa kama mtu asiyependa?
Na mtu huyu atakujibu:
Yaonekana wazi kwamba sina mda kwa kutumia chakula ama kinywaji, lakini ni lazima kwangu kutumia chakula sababu ina mafaa kwa mwili wangu.
Baadaye unamuuliza mtu anayejielekeza nyumbani kwenda kulala:
“Sababu gani unajielekeza kwa kitanda?
Hutambui kwamba kulala ni kupoteza wakati?
Hakuna hata jambo moja utakalotimiza wakati unapolala, hakuna hata kikoroti cha pesa utakalopata wakati unapo lala.”
Mtu huyu atakujibu: Ni lazima nijielekeze nyumbani ili mwili wangu upumzike kwa kulala. Ni lazima nilale.
Baadaye unazungumuzia mtu mwenye kujielekeza hospitalini kwa kwenda kupasuliwa:
Eti wafurahia kwenda hospitalini na kupasuliwa?
Huyu mtu atakujibu, kwa kweli kwa nia yangu singelikubali, bali kupasuliwa kuna mafaa kwa mwili wangu na hata kwa maisha yangu.
Vivyo hivyo, mtu anapashwa kujitahidi kuwa tayari kukutana na Mwenyezi Mungu, sababu yamupasa kwenda kukutana na Mwenyezi Mungu.
5/ Umuhimu ndiwo unaoongoza matendo yetu, umuhimu unatuma sisi kushimama kwa muda na kuwaza kuhusu Mwenyezi Mungu.
Bali, wakati mtu anapozania kuficha zambi zake, kwa kweli anajiziaki mwenyewe.
Anazania mwenyewe kwamba yuko tayari kukutana na Mungu, lakini kwa kweli sivyo.
Kila mmoja wetu anajiona katika hali yake isiyomaanisha namna alivyo.
Je tayari umekwisha kwenda kujifurahisha katika hifadhi ya pumbao, na kuingia katika chumba cha kioo na kujifurahisha kwa kujitazama humo ndani, ukijitazama kwenye vioo mbalimbali:
Kuna kioo kinacho onesha mtu murefu, na kumuonesha kama mtu mfupi.
Kioo kingine kinaonesha mtu munene sana na kumuonesha picha yake kama mtu mgonde sana, na kioo kingine kinaonesha mtu mwembamba sana kuwa na picha sawa mtu munene sana.
Hili ndilo jambo linalotukia wakati mtu anajizania, na hasa wakati mtu anakusudia kufunika zambi zake na kuwa muhukumu anayekosoa wenziwe.
6/ Ni hayo Mwenyezi Mungu anayosema kuhusu mtu yule asiyeshangilia zambi, wala hasukumi mbele zambi iliyo ndani ya mwengine, bali hujaribu kufunika na kuficha zambi iliyo ndani mwake, na kukosoa watu wengine akifunika zambi zake, Mungu anasema kwamba hakuna yule atakaye hepuka ama kutoroka hukumu.
Tusisahau: Hakuna uzuru.
Luka 19: 22
“Akamwambia: Kwa kinywa chako nitakuhukumu, wewe mtumwa mbaya.
Ulijua mimi ni mtu mkali, nikiondoa ile nisiyoweka, nikivuna nisiyopanda;”
Bwana Yesu Kristo anamwambia mtumwa mbaya,
Kwa kinywa chako nitakuhukumu.
Tusisahau kamwe kwamba sawasawa maandiko ya Waroma 2:2 inavyotuambia, hukumu ya Mungu itakuwa ya haki na Mwenyezi Mungu atahukumu kufwatana na masemi ya mtu.
Waroma 14: 10
“Lakini wewe, kwa nini unahukumu ndugu yako?
Na wewe, kwa nini unazarau ndugu yako?
Kwa sababu sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.”
Hata mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba tutatoa hesabu ya masemi yetu, na wao walio katika zambi, wanaoishi zambini, na kufa ndani ya zambi, watahukumiwa sawasawa na yale yaliyotoka vinywani mwao.
Wao peke watajihukumu kwa siku hiyo ya hukumu.
Tafsiri ya musemwa wa mwisho wa aya ya tatu ni kama ifwatavyo:
WEWE HUZANI KWELI KWAMBA UTAHEPUKA?
(nilibadirisha Je “unawaza” nikilibadili na “Unazani kweli” na kwa kweli nina sababu na sheria kufanya hivyo.
Katika Kigriki msingi na china la neno kuwaza latoka kwenye Hesabu, na tafsiri lake ni neno: kuhesabu, kujumulisha, kukadirisha ama kuleta nambari.
Kwa kweli ni neno la hesabu.
Eti wewe ulikaa ukiwaza na kujaribu kufahamu kama waweza kuhepuka na kukimbia, ama kutoroka hukumu?
Kwa kweli, wewe huwezi kamwe.
7/ Tuchunguze kwanza neno “Kutoroka”
Kuna bahati namna ine kwa mwanadamu kutoroka wakati anavunja sheria ya kibinaadamu, ama sheria za watu: bali hali zote zile haziwezekani kwa mtu mwenye kuvunja sheria ya Mwenyezi Mungu.
Jameni muniruhusu niwaoneshe, masemi yangu yanamaanisha nini:
Yawezekana mtu kutenda uhalifu ama maovu bila kuvumbulikana.
Ya pili, yawezekana jambazi anatenda maovu, ajali yake inajulikana wazi, bali ukorofi unaingia katika mashitaki na mahakama yake na yeye anafikia kutoroka.
Ya tatu, hata kama maovu ya jambazi huyo inajulikana, anashikwa na kuelekezwa mahakamani, bali katika mashitaki na kusamba kunapitikana majadiliano kufikia kiwango cha jambazi huyo kuachiliwa.
Na kwa mwisho ni kesi ya jambazi anayenaswa, anapelekwa mahakamani, anasambishwa na kutiwa kwenye gereza, bali baadaye anatoroka.
Bali, kesi hizi zote za kutoroka toka sheria ya wanadamu, haziwezi kamwe kutendeka kwa sheria ya Mwenyezi Mungu.
8/ Katika Zaburi 139: 1 – 10, twasoma:
“Ee Bwana, umenitafuta na kunijua.
Unajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu,
Unafahamu wazo langu toka mbali.
Unatafuta njia yangu na kulala kwangu,
Na unajua njia zangu zote.
Hakuna neno ulimini mwangu
Ambalo hulijui kabisa, Ee Bwana.
Umenivizia nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
Hekima namna hii ni ya ajabu ya kunishinda mimi; Ni juu, siwezi kuifikia.
Niende wapi mbali na Roho yako? Au nikimbie wapi toka uso wako?
Nikipanda mbinguni, wewe ni kule;
Nikifanya kitanda changu katika Hadeze, tazama, wewe ni kule.
Nikitwaa mawingu ya asubui, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
Hata kule mkono wako utaniongoza,
Na mkono wako wa kuume utanishika.”
Hapa, tunajibu za kesi hizo mbili za kwanza zinazo ambatana na wakati maovu iliyotendwa na jambazi haijulikane.
Kwa kweli, Mwenyezi Mungu hufahamu yote juu yako.
Yeye anarikodi mambo yako yote kwa wakati wote.
Anafahamu neno lililo kwa ulimi wako. Anajuwa yote juu yako.
Baadaye anasema:
“Niende wapi mbali na Roho yako? Na Nikimbie wapi toka Uso wako?
Nikipanda mbinguni Wewe ni kule: Nikifanya kitanda changu katika Hadeze, tazama, Wewe ni kule.”
(kwa pande ya upeo wa macho ya Kaskazini, kwa pande ya upeo ya macho ya Kusini).
Nikitwaa mawingu ya asubui,(kumaanisha wakati jua linapoamka Mashariki)
Na kukaa pande za mwisho za bahari;(kumaanisha Mangaribi)
Hata kule mkono wako utaniongoza.”
Hakuna jinsi ya kukimbia Uso wa Mwenyezi Mungu, hakuna namna ya kukimbia mahali pa hukumu yake.
9/ Kesi ya tatu tuliyofikiri ni kwamba, jambazi anayepashwa kuhukumiwa, alipelekwa mahakamani, wakati wa mashitaki yake, majadiliano yalitokea na yaliokoa mtu yule, ama wanasheria wake walitumia ukorofi fulani.
Tufahamu kwamba Maandiko yanatuambia katika kitabu cha
Hesabu 14: 18, kwamba:
“BWANA ni mpole kwa hasira, mwenye kujaa rehema, akisamehe uovu na kosa, na hakika hataachilia wenye makosa; akipatiliza wana kwa uovu wa baba zao katika kizazi cha tatu na cha ine.”
Na hakika hataachilia wenye makosa.
Kesi ya mwisho ni ya jambazi aliyehukumiwa, kiisha akatoroka toka gereza. Kwa kweli, haiwezekani kutoroka hukumu ya Mwenyezi Mungu.
Twasoma katika Luka 16 kwamba huyo mtu mwenye mali mengi hakuweza kutoroka.
Haikuwezekana atoke mahali alipokuwa ili aende kuagiza wandugu zake waliokuwa wangali duniani.
10/ Katika kitabu cha Waroma 2: 4, twaona ni nini Neema ya Kawaida,
“Au unazarau utajiri wa wema wake na saburi na uvumilivu wake, usijue ya kama wema wa Mungu unakupeleka kwa toba?
Neema ya kawaida ni nini?
Uzao wote wa kibinadamu uko katika zambi na hakuna hata kiumbe kimoja chenye kitamudai Mwenyezi Mungu kitu chochote kile.
Baada ya Adam na Awa kuanguka katika zambi, ingelikuwa haki, kama Mwenyezi Mungu angelikusudia kuwashika na kuwatupa ndani ya ziwa la moto.
Wangelipata malipo ya yale waliostahili.
Bali, Mwenyezi Mungu hakuna mtu anayeweza kumudai kitu.
Kwa kweli, kwa vizazi na vizazi, Mungu anaendelea kubariki mwanadamu.
Tuchunguze pamoja kama Neema ya kawaida ni nini?
Kwa mfano:
Kwa sasa wewe haumwamini Bwana Yesu Kristo na unaishi na kwa sasa, wewe si ndani ya ziwa la moto ama Jehenama, hii ni Neema ya kawaida.
Wewe hauko ndani ya Jehenama, unaishi hapa duniani ukiwa na afya nzuri, na katika utajiri. Hii ni neema ya kawaida toka Mwenyezi Mungu.
Unaishi katika gorofa nzuri, gari yako ni maridadi, jamaa lako ni lakupendeza, unatosheka na vyakula na unazunguukwa na vitu virembo. Hii ni neema ya kawaida toka Mungu.
Unatoka kazini na unaelekea kwenye makao yako, unapofika nyumbani, watoto wako wenye afya njema wanakuja kukupokea, hii ni neema ya kawaida toka Mungu.
Wewe unayo uwezo wa kuingiza mkono wako kwenye mfuko na kutowa pesa ndogo ya kumpa mtoto wako kwa shuguli zake, hii ni neema ya kawaida toka Mungu.
Kuwa na uwezo huu wote wewe pekee, siyo haki yako.
Unastarehe ukila chakula kitamu, hii ni neema ya kawaida toka Mungu.
Neema ya kawaida toka Mungu inanyeshe kama nvua ya baraka juu ya watu wasiookoka, wanaishi katika kutosheka na vyote, wakiwa na afya njema, utajiri na uwingi wa vifaa.
Hii ni matokeo ya wema wa Mwenyezi Mungu, na saburi na uvumilivu.
11/ Tutambue ya kwamba aya ya ine ni ulizo:
“Au unazarau utajiri wa wema wake na saburi na uvumilivu wake?”
Na jibu ni kwamba: Kwa kweli ni hivyo unavyo fanya.
Asili ya mwanadamu ni kukosa shukrani kwa Mwenyezi Mungu.
Nikusema; kuzarau, ni kuangalia kitu ukishusha mecho toka juu, kubeula.
Yawezekana mwanadamu kubeula mema ya Mungu akiyaangalia na kushusha mecho toka juu?
Ndiyo ni namna hiyo mambo yanafanyika.
12/ Mara tena kuna ulizo inayopita katika mafikili yetu:
Sababu gani Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wapotevu?
Mwenyezi Mungu anasema wazi kwamba kiini cha utajiri wa wema wake na saburi na uvumilivu wake ni ili Mungu akupeleke kwenye toba.
Kusudi moja ya Mwenyezi Mungu kukukabizi hivyo vifaa vyote, kwa njia ya neema ya kawaida toka kwake, ni ili umukaribiye, uje kwake, umsadiki na kuweka tumaini katika Mwana wake, na umwamini Bwana Yesu Kristo.
13/ KUTUBU ama TOBA
Neno lake la msingi la maanisha mabadiriko ya mafikiri, kuambatanisha mabadiliko kamili iliyo kama gundi inayo miliki mwenendo na hali yetu ya njee, namna watu wanavyotusoma.
Mtu anaacha kujitegemea na kujitizama na anageuza mecho yake kwa Mungu, ndani ya Bwana Yesu Kristo.
14/ Kwa sababu gani watu wanabaki bila wokovu?
Jibu linapatikana kwa aya ya 5, inayosema:
Lakini kwa ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba.
Neno la Kigriki lenye kufasiriya neno “ugumu”, neno lile lilitumiwa na waganga kwa kumaanisha ugonjwa wa ugumu ndani ya mishipa, na kweli sote tunakubaliana kwamba ugonjwa wa ugumu ndani ya mishipa waweza kupeleka mtu kuwa magonjwa sana zaidi, vivyo hivyo, ugumu wa kiroho utakufikisha kwa hali ya ukosefu wa moto rohoni.
15/ Baadaye anatuambia kwamba watu wale wanajiwekea akiba ya hasira ya Mungu,
Wanakuwa wenye ulafi ya hasira ya Mungu.
Picha hapa ni mtu mulafi mwenye kujiwekea akiba tele ya hasira, anakusanya aina zote kubwa za hasira, hana budi ya kufahamu ya kwamba anajitayarisha kwa kukutana na Mungu mwenye atamutupa ndani ya ziwa la moto.
16/ Pole pole, toni moja kwa toni lingine unajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile la hasira na ufunuo wa hukumu ya Mungu.
Kila saa na nyakati lenye ulitupilia neema ya Mungu, unajiwekea nyongezo kwa akiba ya hasira ya Mungu, na hii ndiyo kanuni.
Hukumu ya mtu mwenye hataamini, mtu mwenye hataokolewa itakuwa kwa kadiri alivyoweka hakiba ya hasira ya Mwenyezi Mungu.
Kwa kadiri alivyozarahu wema na neema ya Mungu, ni kwa kadiri hiyo ndivyo anavyofanya akiba ya hasira.
17/ Mwatambua kwamba hukumu ya Mungu ni ya kweli na ya haki, na kwa kadiri ya namna ulivyojibu mbele ya neema ya Mungu.
Kuna kanuni ya tatu ya hukumu, na kanuni hiyo yapatikana katika aya ya sita:
“atakayelipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.”
Ufunuo 20: 11, 12
“Nikaona kiti cha ufalme, kikubwa, cheupe, naye anayeketi juu yake, dunia na mbingu zikakimbia uso wake; na pahali pao hapakuonekana.
Nikaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele ya Mungu, na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, kilicho cha uzima; na wafu wakahukumiwa katika mambo haya yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.”
Hapa twapata kiti cheupe kikubwa cha hukumu, mbele yake wafu wenye zambi wanasimama, wakubwa na wadogo wamesimama mbele ya Mungu, tufahamu kweli kwamba vitabu vikafunguliwa, na wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao.
Kwa kweli, Jehenama itakuwa moto wa kibiriti chenye kuwaka sana kwa yule na zaidi sana kwa yule mwengine.
Jehenama haitakuwa nafasi ya starehe, mambo hayatakuwa raisi, yatakuwa machungu sana kwa yeye aliyejiachilia kuzama kabisa zambini maishani mwake.
Bali, tupime kufikiria jambo moja kwa muda kitambo.
Yaweza kuwa mtu aliyekuwa na maadili safi wakati alipokua akiishi duniani, kufwatana na tabia na mila za watu hapa chini duniani.
Bali, mtu huyu, alipata saa ya kusikiliza Habari Njema na Mwenyezi Mungu alimubariki kweli na vifaa mbalimbali, bali kwa muda huu wote alizarahu neema ya Mungu iliyo ndani ya Mwokozi Yesu Kristo.
Atahukumiwa sawasawa na matendo yake kwa kadiri ya wingi wa akiba ya hasira ya Mungu, yeye alijichungia akiba ya wingi wa hasira ya Mungu.
Wapendwa wapenzi, ninawaomba razi, musijiwekee akiba ya hasira ya Mungu kwa siku hiyo ya hukumu.
Mwenyezi Mungu alituwekea njia ya kuepuka hasira hiyo.
Neema yake, Mapendo yake na Masamaa yake ni ya bure na yapatikana ndani ya Mwana wake wa Pekee, Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Yoane 3: 16
“Kwa maana Mungu alivyopenda ulimwengu, hata kutoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu akimwamini asipotee, lakini apate uzima wa milele.”
AMINA
N°Ref: 11/24/1963/ 263 - COMMON GRACE / 08/19/2022